Zaburi 110 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Hakikisho la ushindi kwa mteule wa MunguYa Daudi. Zaburi.

1 Zab 45:6; Mt 22:44; Mk 12:36; Lk 20:42-43; 1 Kor 15:25; Mdo 2:34-35; Efe 1:20-22; Kol 3:1; Ebr 1:13; 8:1; 10:12-13 Neno la BWANA kwa Bwana wangu,

Uketi upande wangu wa kuume,

Hadi niwafanyapo adui zako

Kuwa chini ya miguu yako.

2BWANA atainyosha toka Sayuni

Fimbo ya nguvu zako.

Uwe na enzi kati ya adui zako;

3 Amu 5:2; Zab 96:9; Mdo 2:41 Watu wako watajitoa kwa hiari,

Siku ya uwezo wako;

Kwa uzuri wa utakatifu,

Tokea tumbo la asubuhi,

Unao umande wa ujana wako.

4 Hes 23:19; Zek 6:13; Ebr 5:6; 6:20; 7:17,21 BWANA ameapa,

Wala hataghairi,

Ndiwe kuhani hata milele,

Kwa mfano wa Melkizedeki.

5 Zab 16:8; 2:5; Rum 2:5; Ufu 11:18 Bwana yu mkono wako wa kuume;

Atawaponda wafalme,

Siku ya ghadhabu yake.

6 Hab 3:13 Atahukumu kati ya mataifa,

Ataijaza nchi mizoga;

Atawaponda wakuu katika nchi nyingi.

7 Isa 61:1; Yn 3:34; Isa 53:12 Atakunywa maji ya mto njiani;

Kwa hiyo atakiinua kichwa chake kwa ushindi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help