Mathayo 8 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Yesu amtakasa mwenye ukoma

1 Mk 1:40-44; Lk 5:12-14 Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.

2Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.

3Yesu akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukatakasika.

4Law 13:49; 14:1-32; Mt 9:30; Mk 7:36; Lk 17:14 Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila nenda zako, ukajioneshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.

Yesu amponya mtumishi wa afisa

5 Lk 7:1-10 Na alipoingia Kapernaumu, afisa mmoja alimjia,Yn 4:47

6akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.

7Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye.

8Yule afisa akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.

9Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.

10Mt 15:28 Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa yeyote katika Israeli.

11Lk 13:29; Isa 49:12; 59:19; Mal 1:11; Zab 107:3 Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Abrahamu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;

12Mt 22:13; 24:51; 25:30; Lk 13:28 bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

13Mt 9:29; 15:28 Naye Yesu akamwambia yule afisa, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona wakati ule ule.

Yesu aponya wengi nyumbani kwa Petro

14 Mk 1:29-34; Lk 4:38-41 Na Yesu alipofika nyumbani kwa Petro, akamwona mkwe wa Petro, mamaye mkewe, amelala kitandani akiugua homa.1 Kor 9:5

15Akamgusa mkono, homa ikamwacha; naye akaondoka, akawatumikia.

16Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa wagonjwa,

17Isa 53:4 ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,

Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu,

Na kuyachukua magonjwa yetu.

Watakaokuwa wafuasi wa Yesu

18 Mk 4:35; Lk 8:22 Naye Yesu alipoona makutano mengi wakimzunguka, aliamuru kuvuka kwenda ng'ambo.

19Lk 9:57-60 Mwandishi mmoja akamwendea, akamwambia, Mwalimu, nitakufuata kokote uendako.

202 Kor 8:9 Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota; lakini Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.

211 Fal 19:20 Mwingine katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, nipe ruhusa kwanza, niende nikamzike baba yangu.

22Yn 1:43; 5:25; Rum 6:13 Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao.

Yesu atuliza dhoruba

23 Mk 4:36-41; Lk 8:23-25 Akapanda katika mashua, wanafunzi wake wakamfuata.Zab 4:8

24Kukawa na msukosuko mkuu baharini, hata mashua ikafunikwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi.

25Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia.

26Mt 14:31; 16:8 Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu.

27Wale watu wakahamaki wakisema, Huyu ni mtu wa namna gani hata pepo na bahari zamtii?

Yesu awaponya Wagadara wenye pepo

28 Mk 5:1-17; Lk 8:26-37 Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagadara, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wakitoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile.

29Lk 4:41; 2 Pet 2:4 Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya wakati wetu?

30Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakila.

31Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe.

32Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakateremka kwa kasi gengeni hadi baharini, wakafa maji.

33Lakini wachungaji walikimbia, wakaenda zao mjini, wakazieneza habari zote na habari za wale wenye pepo pia.

34Na tazama, mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; nao walipomwona, walimsihi aondoke katika nchi yao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help