Zaburi 6 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Sala ya kuponywa ugonjwa hatariKwa mwimbishaji: kwa ala za muziki zenye nyuzi; kulingana na mtindo wa Sheminithi. Zaburi ya Daudi.

1 Zab 38:1 BWANA, usinikemee kwa hasira yako,

Wala usinirudi kwa ghadhabu yako.

2 Hos 6:1 BWANA, unifadhili, maana ninanyauka;

BWANA, uniponye, mifupa yangu imefadhaika.

3 Mit 18:14; Mt 26:38 Na nafsi yangu imefadhaika sana;

Na Wewe, BWANA, hadi lini?

4BWANA urudi, uniopoe nafsi yangu,

Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.

5 Zab 30:9 Maana mautini hapana kumbukumbu lako;

Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?

6Nimechoka kwa kuugua kwangu;

Kila usiku nakibubujikia kitanda changu;

Nililowesha godoro langu kwa machozi yangu.

7Macho yangu yameharibika kwa masumbufu,

Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi.

8 Mt 7:23; Lk 13:27 Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu;

Kwa kuwa BWANA ameisikia sauti ya kilio changu.

9 Zab 3:4; 31:22; 40:1,2 BWANA ameisikia dua yangu;

BWANA atayatakabali maombi yangu.

10Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika,

Watarudi nyuma, kwa ghafla wataaibika.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help