Obadia UTANGULIZI - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

UTANGULIZIMaana ya jina Obadia katika lugha ya Kiebrania ni “mtumishi wa BWANA” au “mwabudu BWANA”. Kitabu hiki hakitaji kiliandikwa lini, aidha mwandishi alipoishi sio yakini na mambo kadhaa ya ujumbe wake yanasimuliwa katika vitabu vingine vya manabii.Ujumbe wa Obadia unahusu taifa la Edomu. Edomu maana yake ni “nyekundu” nalo ni jina aliloitwa Esau, wazao wake na nchi walimoishi (Mwa 36:1,8-9; 25:15,30). Kwa kuwa Israeli ilitawala Edomu baadaye Waedomi wakajikomba kulikuweko kutoelewana hata uhasama. Yuda ilipotekwa, Yerusalemu ukabomolewa, wakazi wake wakachukuliwa mateka, Edomu walifurahi wakajiunga na maadui wa Yuda kupora mali ya Yuda. Ujumbe wa nabii Obadia unaeleza hali ya uhasama na mafarakano yaliyokuwapo kati ya mataifa ndugu. Pia ukatoa hukumu ya Mungu kwa Edomu. “Siku ya BWANA” ni wakati ambapo taifa la Mungu litalipiza kisasi kwa Edomu.Yaliyomo:1. Mungu atashusha kiburi cha Edomu, Aya 1-42. Mungu ataangamiza nchi ya Edomu, Aya 5-93. Sababu za kuangamizwa Edomu, Aya 10-164. Israeli na Yuda wataimarishwa, Aya 17-21
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help