Zaburi 51 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Sala ya utakaso na msamahaKwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi, wakati Nabii Nathani alipomjia, alipokuwa amekwisha kwenda kwa Bathsheba

1 Kol 2:14 Ee Mungu, unirehemu,

Sawasawa na fadhili zako.

Kiasi cha wingi wa rehema zako,

Uyafute makosa yangu.

2 Eze 36:25; Zek 13:1; 1 Kor 6:11; Ebr 9:14; 1 Yoh 1:7; Ufu 1:5 Unioshe kabisa uovu wangu,

Unitakase dhambi zangu.

3 Zab 32:5 Maana nimejua mimi makosa yangu

Na dhambi yangu iko mbele yangu daima.

4 Rum 3:4; Lk 15:21; Mwa 39:9 Nimekutenda dhambi Wewe peke yako,

Na kufanya maovu mbele za macho yako.

Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo,

Na kuwa safi utoapo hukumu.

5 Ayu 14:4; Yn 3:6; Rum 5:12 Tazama, nilizaliwa nikiwa na hatia;

Mama yangu alinichukua mimba nikiwa na dhambi.

6Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni;

Nawe utanifundisha hekima kwa siri,

7Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi,

Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.

8Unifanye kusikia furaha na shangwe,

Mifupa uliyoiponda ifurahi.

9Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu;

Uzifute hatia zangu zote.

10 Mit 20:9; Yer 13:27; Eze 11:19; Mdo 15:9; Efe 2:10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi,

Uifanye upya na kuithibiti roho yangu.

11 Mwa 4:14; Eze 36:27; Rum 8:9 Usinitenge na uso wako,

Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.

12 Rum 8:15; 2 Kor 3:17 Unirudishie furaha ya wokovu wako;

Unitegemeze kwa roho ya upendo.

13Nitawafundisha wakosaji njia zako,

Na wenye dhambi watarejea kwako.

14Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu,

Uniponye na umwagaji wa damu,

Na ulimi wangu utaiimba haki yako.

15Ee Bwana, uifumbue midomo yangu,

Na kinywa changu kitazinena sifa zako.

16Maana hupendezwi na dhabihu, na kama ningeitoa,

Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa.

17Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika;

Moyo uliovunjika na kupondeka,

Ee Mungu, hutaudharau.

18Uitendee mema Sayuni kwa radhi yako,

Uzijenge kuta za Yerusalemu.

19 Mal 3:3 Ndipo utakapopendezwa na dhabihu za haki,

Na sadaka za kuteketezwa, na kafara.

Ndipo watakapotoa ng'ombe

Juu ya madhabahu yako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help