1 kimwili.
6Lutu akawatokea mlangoni, akafunga mlango nyuma yake.
7Akasema, Basi, nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi.
8Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua mwanamume, nawasihi nitawatolea kwenu mkawafanyie vilivyo vyema machoni penu, ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa wamekuja chini ya dari yangu.
9
23Jua lilikuwa limechomoza juu ya nchi Lutu alipoingia Soari.
24Mt 10:15; 11:23-24; Lk 10:12; 17:29; 2 Pet 2:6; Yud 1:7; Kum 29:23; Zab 11:6; Isa 13:19; Yer 20:16; 50:40; Eze 16:49,50; Hos 11:8; Amo 4:11; Sef 2:9 Ndipo BWANA akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto kutoka mbinguni kwa BWANA.
25Mwa 14:3; Zab 107:34 Akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na wote waliokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile.
26Lk 17:32 Lakini mkewe Lutu, akiwa nyuma ya mumewe, aliangalia nyuma akawa nguzo ya chumvi.
27 Mwa 18:22 Abrahamu akatoka asubuhi kwenda mahali aliposimama mbele za BWANA,
28Ufu 18:9 naye akatazama upande wa Sodoma na Gomora na nchi yote ya hilo Bonde, akaona, na tazama, moshi wa nchi ukapanda, kama moshi wa tanuri.
29Mwa 8:1; 18:23 Ikawa Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Abrahamu, akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu.
Asili ya Wamoabi na Waamoni30 Mwa 19:17,19 Lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake wawili.
31Mwa 16:2,4; 38:8; Kum 25:5 Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mwanamume katika nchi atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote.
32Lk 21:34; 1 Kor 15:33; Mk 12:19 Haya, na tumnyweshe baba yetu mvinyo, tukalale naye, ili tumhifadhie baba yetu uzao.
33Wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.
34Ikawa siku ya pili, mkubwa akamwambia mdogo, Tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe mvinyo tena usiku huu, ukaingie ukalale naye ili tupate uzao kwa baba yetu.
35Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.
36Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao.
37Kum 2:9 Yule mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo.
38Kum 2:19 Na yule mdogo naye akazaa mwana akamwita jina lake Benami; huyo ndiye baba wa Waamoni hata leo.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.