Zaburi 41 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Hakikisho la msaada wa Mungu na ombi la uponyajiKwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1

BWANA atamwokoa siku ya taabu.

2BWANA atamlinda na kumhifadhi hai,

Naye atafanikiwa katika nchi;

Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake.

3BWANA atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani.

Katika ugonjwa wake unamponya maradhi yake yote.

4 Zab 6:2 Nami nilisema, BWANA, unifadhili,

Uniponye roho yangu maana nimekutenda dhambi.

5Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya,

Atakufa lini, jina lake lipotee?

6 Zab 12:2 Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo,

Moyo wake hujikusanyia maovu,

Naye atokapo nje huyanena.

7Wote wanaonichukia wananong'onezana juu yangu,

Wananiwazia yaliyo mabaya zaidi.

8Wanafikiri pigo liualo limemshika,

Akalala asiweze kusimama tena.

9 Mt 26:23; Oba 1:7; Mk 14:18; Lk 22:21; Yn 13:18 Hata rafiki yangu mwandani niliyemtumaini,

Aliyekula pamoja nami,

Ameniinulia kisigino chake.

10Lakini Wewe, BWANA, unifadhili,

Uniinue nipate kuwalipa.

11Kwa neno hili nimejua ya kuwa wapendezwa nami,

Kwa kuwa adui yangu hajivunii kunishinda.

12 Zab 34:15; Mdo 2:28 Nami katika ukamilifu wangu umenitegemeza,

Umeniweka mbele za uso wako milele.

* * *

13 Zab 106:48 Na atukuzwe BWANA, Mungu wa Israeli,

Tangu milele hata milele. Amina na Amina.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help