Mwanzo 4 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Kaini amwua Habili

1Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto wa kiume kwa msaada wa BWANA.

2Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima.

3Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA.

4 Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua.

9BWANA akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, kwani mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?

10Ebr 12:24; Ufu 6:10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.

11Kum 28:15-20; Gal 3:10; Ayu 16:18 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kutoka kwako;

12utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na makao duniani.

13Kaini akamwambia BWANA, Adhabu yangu imeniwia kubwa, haichukuliki.

14Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na makao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.

15Eze 9:4,6 BWANA akamwambia, Kwa sababu hiyo yeyote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. BWANA akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.

16 2 Fal 13:23; 24:20; Yer 23:39; 52:3 Kaini akatoka mbele za uso wa BWANA, akakaa katika nchi ya Nodi, Mashariki mwa Edeni.

Wazawa wa Kaini

17 Zab 49:11 Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Henoko; akajenga mji akauita Henoko, kwa jina la mwanawe.

18Henoko akamzaa Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli; Mehuyaeli akamzaa Methushaeli; Methushaeli akamzaa Lameki.

19Lameki akajitwalia wake wawili, jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila.

20Ada akamzaa Yabali; huyo ndiye baba yao wakaao katika hema na kufuga wanyama.

21Na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo ndiye baba ya wote wapigao kinubi na filimbi.

22Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma; na dada yake Tubal-kaini alikuwa Naama.

23Lameki akawaambia wake zake,

Sikieni sauti yangu, Ada na Sila;

Enyi wake za Lameki, sikilizeni ninachosema;

Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha;

Kijana kwa kunichubua;

24Kama Kaini akilipiwa kisasi mara saba,

Hakika Lameki atalipiwa mara sabini na saba.

Kuzaliwa kwa Sethi

25Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua.

26Mwa 6:2; 1 Fal 18:24; Zab 116:17; Yoe 2:32; Sef 3:9; Yn 1:12; Mdo 15:17; 1 Kor 1:2 Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la BWANA.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help