Yoshua Mwana wa Sira 49 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Yosia na Wastahiki wengine

1 2 Fal 22:1,11-13; 23:3,25 Ukumbusho wa Yosia ni kama ubani

Uliochanganywa kwa kazi ya fundi;

Ni tamu kama asali kinywani,

Kama wimbo kwenye karamu ya mvinyo.

2Akawa adili katika kuwaongoza watu,

Akayakomesha machukizo ya ubatili;

3Akaweka moyo wake sawa kama BWANA,

Siku za uovu akashindisha utauwa.

Wafalme na manabii wa mwisho

4Isipokuwa ni Daudi na Hezekia na Yosia, wote walifanya kukosa; kwa maana waliiacha sheria yake Aliye Juu; naam, wale wafalme wa Yuda wote pia.

5Wakawapa wengine nguvu zao, na kuutoa utukufu wao kwa taifa la wageni.

6Yer 1:4-10; 39:8 Mji mtakatifu wakaufanya kuchomwa moto, na njia zake kuwa ganjo,

7kama ilivyoandikwa kwa mkono wake Yeremia. Na huyo naye walimtenda mabaya, ingawa alitakaswa tumboni ili awe nabii, kung'oa, na kutesa, na kuangamiza, kadhalika na kujenga, na kupanda.

8Eze 1:3-15; 14:14-20 Ndiye Ezekieli aliyeona njozi ya utukufu, akaeleza namna ya gari la makerubi.

9Tena nitamtaja Ayubu, nabii aliyezishika njia zote za haki.

10Pia na Manabii Kumi na Wawili, kumbukumbu lao na libarikiwe; hata na mifupa yao ifanikiwe panapo makao yao. Kwa kuwa walimrudishia Yakobo afya yake, na kuwaokoa watu kwa sabiki ya uthabiti wa taraja lao.

Zerubabeli na Yeshua

11 Ezr 3:2; Hag 2:23 Twawezaje kumwadhimisha Zerubabeli? Mradi alikuwa kama mhuri wa pete juu ya mkono wa kuume;

12Hag 1:1,12 kadhalika naye pia Yeshua mwana wa Yesedeki; ambao hao wawili katika siku zao waliijenga nyumba, wakaliinua hekalu takatifu kwa BWANA, lililowekewa utukufu wa daima.

Nehemia

13 Neh 6:15 Naye Nehemia, ukumbusho wake ni mtukufu; alituinulia kuta zilizobomolewa, akatujengea tena nyumba zetu, akayasimamisha malango na makomeo.

Kumbukumbu ya Zamani

14Hakika yake ni wachache ulimwenguni walioumbwa mfano wa Henoko; ambaye yeye naye alichukuliwa juu aingie mbele za uso wa Mungu.

15Wala hakuzaliwa mtu mfano wa Yusufu; naam, mifupa yake ilihifadhiwa.

16Shemu na Sethi wametukuzwa katika wanadamu; na juu ya kila kilicho hai ni utukufu wake Adamu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help