1 Ukuta wakamilika
15Basi huo ukuta ukakamilika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa Eluli, katika muda wa siku hamsini na mbili.
16Neh 2:10; 4:1; 6:1; Zab 126:2 Ikawa adui zetu wote waliposikia, ndipo wamataifa wote waliotuzunguka wakaogopa, nao wakakata tamaa sana machoni pao wenyewe; maana waliitambua kazi hiyo ilivyotendwa na Mungu wetu.
17Tena siku zile wakuu wa Yuda walimtumia nyaraka nyingi Tobia nazo nyaraka za Tobia ziliwafikia.
18Kwa maana walikuwa watu wengi katika Yuda waliomwapia, kwa sababu alikuwa mkwewe Shekania, mwana wa Ara; naye Yehohanani mwanawe amemwoa binti Meshulamu, mwana wa Berekia.
19Tena waliyanena mema yake mbele yangu, na kumwambia maneno yangu. Tobia naye akaniletea mimi nyaraka za kuniogofya.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.