1 Wakorintho 2 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Kumtangaza Kristo aliyesulubiwa

1 1 Kor 1:17 Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubirie siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima.

2Gal 6:14 Maana niliazimu nisijue neno lolote kwenu ila Yesu Kristo, na yeye aliyesulubiwa.

3Mdo 18:9; 2 Kor 10:1 Nami nilikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na kwa kutetemeka sana.

4Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,

5Efe 1:17; 1 The 1:5 ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.

Hekima ya kweli ya Mungu

6 Flp 3:15 Lakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika;

7Rum 16:25 bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;

8Lk 23:34; Yak 2:1; Kol 1:26 ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulubisha Bwana wa utukufu.

9Isa 64:4 Lakini, kama ilivyoandikwa,

Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia,

(Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,)

Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.

10 Mt 13:11; Mit 20:27 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.

11Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.

12Yn 16:13,14 Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.

131 Kor 1:4 Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.

14Yn 8:47; 14:17 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.

151 Yoh 2:20 Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.

16Isa 40:13; Rum 11:34 Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help