Zaburi 129 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Sala ya kushindwa kwa adui za IsraeliWimbo wa Kupanda mlima

1 Eze 23:3; Hos 2:15 Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu,

Israeli na aseme sasa,

2Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu,

Lakini hawakuniweza.

3 Ebr 11:36 Wakulima wamelima mgongoni mwangu,

Wamefanya mirefu mifuo yao.

4 2 The 1:6 BWANA ndiye mwenye haki,

Amezikata kamba zao wasio haki.

5Na waaibishwe, warudishwe nyuma,

Wote wanaoichukia Sayuni.

6 Zab 37:2; Yer 17:5-6 Na wawe kama majani ya darini

Yanyaukayo kabla hayajamea.

7Ambayo mvunaji haujazi mkono wake,

Wala mfunga miganda kifua chake.

8 Rut 2:4; Zab 118:26 Wapitao nao hawasemi, Amani ya BWANA ikae nanyi,

Twawabariki kwa jina la BWANA.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help