Zaburi 130 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Kusubiri wokovu wa MunguWimbo wa kupanda mlima.

1 Omb 3:55; Yon 2:2 Ee BWANA, toka vilindini nimekulilia.

2Bwana, uisikie sauti yangu.

Masikio yako na yaisikilize

Sauti ya dua zangu.

3 Zab 143:2; Yn 8:7-9; Rum 3:20 BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu,

Ee Bwana, nani angesimama?

4 2 The 1:6; Zab 37:2; Yer 17:6; Kut 34:7; Efe 1:7; 1 Fal 8:40; Yer 33:8,9; Ebr 12:28 Lakini kwako kuna msamaha,

Ili Wewe uogopwe.

5 Isa 26:8 Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja,

Na neno lake nimelitumainia.

6Nafsi yangu inamngoja Bwana,

Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi,

Naam, walinzi waingojao asubuhi.

7 Isa 55:7 Ee Israeli, umtarajie BWANA;

Maana kwa BWANA kuna fadhili,

Na kwake kuna ukombozi mwingi.

8 Mt 1:21; Tit 2:14 Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help