Zaburi 71 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Sala ya ulinzi wa daima na msaada

1Nimekukimbilia Wewe, BWANA,

Nisiaibike milele.

2Kwa haki yako uniponye, uniponye,

Unitegee sikio lako, uniokoe.

3 Zab 44:4 Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu,

Ngome imara ya wokovu wangu.

Maana wewe,

Ndiwe mwamba wangu na ngome yangu.

4Ee Mungu wangu, uniponye mkononi mwa mkorofi,

Katika mkono wake mwovu na mdhalimu,

5 Yer 17:7; Rum 15:13 Maana ndiwe tegemeo langu, Ee Bwana MUNGU,

Tumaini langu tokea ujana wangu.

6 Zab 22:9; Isa 46:3; Yer 3:4 Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa,

Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu,

Ninakusifu Wewe daima.

7 Isa 8:18; Zek 3:8; 1 Kor 4:9 Nimekuwa kioja kwa watu wengi,

Lakini wewe ndiwe kimbilio langu la nguvu.

8Kinywa changu kitajazwa sifa zako,

Na heshima yako mchana kutwa.

9Usinitupe wakati wa uzee,

Nguvu zangu zipungukapo usiniache.

10 2 Sam 17:1; Mt 27:1 Kwa maana adui zangu husema juu yangu,

Nao wanaotaka kuniua hushauriana.

11Wakisema, Mungu amemwacha,

Mfuatieni, mkamateni, hakuna wa kumponya.

12 Zab 22:11; 35:22; 70:1 Ee Mungu, usiwe mbali nami;

Ee Mungu wangu, fanya haraka kunisaidia.

13 Zab 35:4; 40:14 Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu.

Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya.

14Lakini mimi nitakutumainia daima,

Nitaendelea kukusifu zaidi na zaidi.

15 Zab 35:28; 40:5 Lakini mimi nitakutumainia daima

Na nitaendelea kukusifu zaidi na zaidi.

16 Zek 10:12; Efe 3:16; Flp 4:13; 2 Tim 2:1 Nitakuja na mambo ya ajabu ya Bwana MUNGU;

Nitawakumbusha watu haki yako Wewe peke yako.

17Ee Mungu, umenifundisha tokea ujana wangu;

Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata leo.

18Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi,

Ee Mungu, usiniache.

Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako,

Na kila atakayekuja uweza wako.

19 Zab 57:10; Mit 24:7; Isa 5:16; Kut 15:11; Zab 35:10; Isa 40:18,25 Na haki yako, Ee Mungu,

Imefika juu sana.

Wewe uliyefanya mambo makuu;

Ee Mungu, ni nani aliye kama Wewe?

20 Zab 60:3; Hos 6:1 Wewe, uliyetuonesha mateso mengi, mabaya,

Utatuhuisha tena.

Utatupandisha juu tena

Tokea pande za chini ya nchi.

21Laiti ungeniongezea ukuu!

Urejee tena na kunifariji moyo.

22 2 Fal 19:22; Isa 60:9 Nami nitakushukuru kwa kinanda,

Na kweli yako, Ee Mungu wangu.

Nitakuimbia Wewe kwa kinubi,

Ee Mtakatifu wa Israeli.

23 Zab 103:4 Midomo yangu itafurahi sana nikuimbiapo,

Na nafsi yangu uliyoikomboa.

24Ulimi wangu nao utasimulia

Haki yako mchana kutwa.

Kwa maana wameaibishwa,

Wametahayarika, wanaonitakia mabaya.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help