Mathayo 27 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Yesu aletwa mbele ya Pilato

1 wakamkusanyikia kikosi kizima.

28Wakamvua nguo, wakamvika vazi jekundu.

29Wakasokota taji la miiba, wakaliweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kuume; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi!

30Isa 50:6 Kisha wakamtemea mate, wakautwaa ule mwanzi, wakampigapiga kichwani.

31Mk 15:20-41; Lk 23:26,33-49; Yn 19:16-30 Walipokwisha kumdhihaki, wakalivua lile vazi, wakamvika mavazi yake, wakamchukua kumsulubisha.

Yesu asulubiwa

32Walipokuwa wakitoka, wakamwona mtu Mkirene, jina lake Simoni; huyu wakamshurutisha auchukue msalaba wake.

33Na walipofika mahali paitwapo Golgotha, yaani, Fuvu la Kichwa,

34Zab 69:22 wakampa kunywa divai iliyochanganyika na nyongo; lakini yeye alipoionja hakutaka kunywa.

35Zab 22:19 Walipokwisha kumsulubisha, waligawana mavazi yake, kwa kupiga kura;

36Wakaketi, wakamlinda huko.

37Wakaweka juu ya kichwa chake mashitaka yake, yaliyoandikwa HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI.

38Isa 53:12 Wakati huo huo wanyang'anyi wawili wakasulubiwa pamoja naye, mmoja katika mkono wake wa kulia, na mmoja katika mkono wake wa kushoto.

39Zab 22:8; 109:25 Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisatikisa vichwa vyao, wakisema,

40Mt 26:61; Yn 2:19 Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, shuka msalabani.

41Kadhalika na wale wakuu wa makuhani wakamdhihaki pamoja na waandishi na wazee, wakisema, Aliokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe.

42Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini.

43Zab 22:9 Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu.

44Pia wale wanyang'anyi waliosulubiwa pamoja naye walimshutumu vile vile.

Kifo cha Yesu

45Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hadi saa tisa.

46Zab 22:2 Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?

47Na baadhi yao waliokuweko, waliposikia, walisema, Huyu anamwita Eliya.

48Zab 69:22 Mara mmoja wao akaenda mbio, akatwaa sifongo, akaijaza siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha.

49Wale wengine wakasema, Acha; na tuone kama Eliya anakuja kumwokoa.

50Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.

51 Kut 26:31-33; Ebr 10:19,20 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hadi chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;

52makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;

53Mdo 26:23; Dan 12:2 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.

54Basi yule afisa, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la ardhi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.

55Lk 8:2-3 Palikuwa na wanawake wengi pale wakitazama kwa mbali, hao ndio waliomfuata Yesu toka Galilaya, na kumtumikia.

56Mt 20:20 Miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yusufu, na mama yao wana wa Zebedayo.

Kuzikwa kwa Yesu

57 Mk 15:42-47; Lk 23:50-55; Yn 19:38-42 Na ilipokuwa jioni akafika mtu tajiri wa Arimathaya, jina lake Yusufu, naye mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa Yesu;Kut 34:25

58mtu huyu alimwendea Pilato akaomba apewe mwili wa Yesu. Ndipo Pilato akaamuru apewe.

59Yusufu akautwaa mwili, akauzongazonga katika sanda ya kitani safi,

60Isa 53:9 akauweka katika kaburi lake jipya, alilokuwa amelichonga mwambani; akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.

61Na pale walikuwapo Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, wameketi kulielekea kaburi.

Ulinzi katika kaburi

62Hata siku ya pili, ndiyo iliyo baada ya Maandalio, wakuu wa makuhani, na Mafarisayo wakamkusanyikia Pilato,

63Mt 16:21; 27:40; 12:40; 17:23; 20:19; Mk 8:31; 9:31; 10:33-34; Lk 9:22; 18:31-33 wakasema, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa angali hai, Baada ya siku tatu nitafufuka.

64Basi amuru kwamba kaburi lilindwe salama hadi siku ya tatu; wasije wanafunzi wake wakamwiba, na kuwaambia watu, Amefufuka katika wafu; na udanganyifu wa mwisho utapita ule wa kwanza.

65Pilato akawaambia, Mna askari; nendeni mkalilinde salama kadiri mjuavyo.

66Dan 6:17 Wakaenda, wakalilinda kaburi salama, kwa kulitia lile jiwe mhuri, pamoja na kuwaweka wale askari walinzi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help