1Baada ya hayo Yesu alijidhihirisha tena kwa wanafunzi wake, penye bahari ya Tiberia, naye alijidhihirisha hivi.
2 kuliko hawa? Akamwambia, Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu.
161 Pet 5:2,4 Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo wangu.
17Yn 13:38; 16:30 Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.
18 Mt 16:22; 26:39 Akasema, Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka.
19Yn 13:36 Akasema neno hilo kwa kuonesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu. Naye akiisha kusema hayo akamwambia, Nifuate.
Yesu na manafunzi aliyempenda20 Yn 13:23 Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu anawafuata; (ndiye huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana, ni nani akusalitiye?)
21Basi Petro akamwona huyo, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu je?
22Yesu akamwambia, Ikiwa nataka huyu akae hata nitakapokuja, imekuhusuje wewe? Wewe unifuate mimi.
23Basi neno hilo lilienea katikati ya ndugu ya kwamba mwanafunzi yule hafi. Lakini Yesu hakumwambia ya kwamba hafi; bali, Ikiwa nataka huyu akae hata nitakapokuja, imekuhusuje wewe?
24 Yn 15:27 Huyu ndiye yule mwanafunzi ayashuhudiaye haya, na aliyeyaandika haya: nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli.
25 Yn 20:30 Pia kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.