1 Mdo 13:19 BWANA, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang'oa mataifa mengi watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe;
2Yos 6:17; 11:11; Kut 23:32; Yos 2:14; Amu 1:24; 2:2 wakati BWANA, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao;
3Yos 23:12; 1 Fal 11:2; Ezr 9:2 binti yako usimwoze kwao wala mtoto wako wa kiume kuoa kwao.
4Kwa kuwa atamkengeusha mwanao asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya BWANA juu yenu, naye atakuangamiza upesi.
5Kum 12:3; Kut 23:24; 34:13 Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomoeni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga.
6 Kut 19:5; Kum 4:20; 14:2; 26:18; Tit 2:14; 1 Pet 2:9; Zab 50:5; Yer 2:3; Amo 3:2; 1 Kor 6:19,20; Zab 135:4 Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako; BWANA Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.
7BWANA hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwa sababu mlikuwa wengi kuliko mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote;
8Kut 32:13; Zab 105:8; Lk 1:55; Kut 13:3 bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kukitimiza kiapo chake alichowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri.
9Kut 20:5-6; 34:6-7; Hes 14:18; Kum 5:9-10; Isa 49:7; 1 Kor 1:9; 10:13; 2 Kor 1:18; 1 The 5:24; 2 Tim 2:13; Ebr 11:11; 1 Yoh 1:9; Neh 1:5; Dan 9:4 Basi jueni ya kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hadi vizazi elfu;
10naye huwalipa wamchukiao mbele ya uso wao, kuwaangamiza. Hatakuwa mlegevu kwake yeye amchukiaye, atamlipa mbele ya uso wake.
11Zab 21:8; Mit 11:31; Isa 59:18; Nah 1:2; Rum 12:19 Basi zishike amri, na sheria, na hukumu ninazokuamuru leo, uzitende.
Baraka za utiifu12 Kum 11:13-17 Na itakuwa, kwa sababu mnazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi BWANA, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako;
13Kut 23:25; Zab 1:3; 11:7; Mit 15:9; Yn 14:21; 1 Yoh 2:5 naye atakupenda na kukubariki na kukuongeza tena ataubariki uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, nafaka zako na divai yako, na mafuta yako, kuongezeka kwa ng'ombe na kondoo wako, katika nchi aliyowaapia baba zako kuwa atakupa.
14Utabarikiwa kuliko mataifa yote; hakutakuwa na mwanamume wala mwanamke aliye tasa kati yenu; wala kati ya wanyama wenu wa kufugwa.
15Kut 9:14; 15:26; Kum 28:27; Zab 105:37 Na BWANA atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yoyote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao.
16Amu 8:27; Zab 106:36 Nawe angamiza mataifa yote atakayokupa BWANA, Mungu wako; jicho lako lisiwahurumie, wala usiitumikie miungu yao; kwani jambo hilo litakuwa ni mtego kwako.
17Hes 33:53 Nawe kama ukisema moyoni mwako, Mataifa haya ni mengi kuliko mimi; nitawatoaje katika milki yao?
18Amu 6:13; Zab 77:11; 105:5; 135:8-10; Isa 63:11-15 Usiwaogope; kumbuka sana BWANA, Mungu wako, alivyomfanya Farao na Misri yote;
19uyakumbuke hayo majaribu makuu yaliyoyaona macho yako, na hizo ishara, na maajabu, na mkono wa nguvu, na mkono ulionyoka, aliokutolea nje BWANA, Mungu wako; ndivyo atakavyowafanya BWANA, Mungu wako, mataifa yote unaowaogopa.
20Kut 23:28; Yos 24:12 Tena BWANA, Mungu wako, atapeleka mavu kati yao, hata hao watakaosalia, hao wajifichao, waangamie mbele zako.
21Hes 14:9; 16:3; Yos 3:10; Kum 10:17; Neh 1:5; 4:14; 9:32 Usiingiwe na hofu kwa sababu yao; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yuko pamoja nawe, Mungu mkuu, mwenye utisho.
22Naye BWANA, Mungu wako, atayatupilia mbali mataifa yale mbele yako kidogo kidogo; haikupasi kuwaangamiza kwa mara moja, wasije wakaongezeka kwako wanyama wa mwitu.
23Ila BWANA, Mungu wako, atawatoa mbele yako, atawatia mashaka, mashaka makuu, hata waishe kuangamizwa.
24Yos 10:24; 12:1; Kum 11:25; Yos 1:5; 10:8; 23:9 Na wafalme wao atakutilia mkononi mwako, nawe utalipoteza jina lao litoke chini ya mbingu; hapana mtu atakayeweza kusimama mbele yako, hata utakapokwisha kuwaangamiza.
25Kut 32:20; Kum 12:3; 1 Nya 14:12; Kut 20:17; Yos 7:1; Lk 12:15; Kol 3:5; Amu 8:27; Sef 1:3; Kum 17:1 Sanamu za kuchonga za miungu yao mtaziteketeza kwa moto; usitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala usiitwae iwe yako usije ukanaswa nayo; kwa maana ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako;
26Law 27:28; Yos 6:17 na usitie kitu kilicho haramu ndani ya nyumba yako, usije ukalaaniwa kama haramu hiyo; ukichukie kabisa na kukikataa kabisa, kwa kuwa ni kitu kilicholaaniwa.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.