Zaburi 115 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Unyonge wa sanamu na ukuu wa Mungu

1 Isa 48:11; Eze 36:32 Ee BWANA, kutukuza usitutukuze sisi,

Bali ulitukuze jina lako,

Kwa ajili ya fadhili zako,

Kwa ajili ya uaminifu wako.

2 Zab 42:3,10; 79:10; Yoe 2:17 Kwa nini mataifa kusema,

Yuko wapi Mungu wao?

3 1 Nya 16:26; Zab 135:6; Dan 4:35 Lakini Mungu wetu yuko mbinguni,

Alitakalo lote amelitenda.

4 Kum 4:28; Zab 135:15-18; Isa 40:19; Yer 20:3; Hos 8:6; 1 Kor 10:19,20; Ufu 9:20 Sanamu zao ni fedha na dhahabu,

Kazi ya mikono ya wanadamu.

5Zina vinywa lakini hazisemi,

Zina macho lakini hazioni,

6Zina masikio lakini hazisikii,

Zina pua lakini hazinusi harufu,

7Zina mikono lakini hazishiki,

Zina miguu lakini haziendi,

Wala hazitoi sauti kwa koo zao.

8 Zab 135:18; Isa 44:9,10; Yon 2:8; Hab 2:18 Wazitengenezao watafanana nazo,

Sawa na wote wanaozitumainia.

9 Zab 33:20; Mit 30:5 Enyi Israeli, mtumainini BWANA;

Yeye ni msaada wao na ngao yao.

10 Mal 2:7 Enyi mlango wa Haruni, mtumainini BWANA;

Yeye ni msaada wao na ngao yao.

11Enyi mmchao BWANA, mtumainini BWANA;

Yeye ni msaada wao na ngao yao.

12 Efe 1:3 BWANA ametukumbuka,

Naye atatubariki sisi.

Ataubariki mlango wa Israeli,

Ataubariki mlango wa Haruni,

13 Law 26:3; Kum 11:27; Zab 24:4; Mit 10:6; Ufu 11:18; 19:5 Atawabariki wamchao BWANA,

Wadogo kwa wakubwa.

14BWANA na awaongeze ninyi,

Ninyi na watoto wenu.

15 Mwa 14:19; 1:1; Zab 96:5 Na mbarikiwe ninyi na BWANA,

Aliyezifanya mbingu na nchi.

16Mbingu ni mbingu za BWANA,

Bali nchi amewapa wanadamu.

17Wafu hawamsifu BWANA,

Wala yeyote ashukaye kwenye kimya;

18 Zab 145:2; Dan 2:20 Bali sisi tutamhimidi BWANA,

Tangu leo na hata milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help