Habakuki UTANGULIZI - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

UTANGULIZIKitabu hiki kinazungumzia suala la mateso, dhambi na haki ya Mungu kama ilivyo kwa Ayubu na Zaburi ya 73. Habakuki anaanza kwa kumlalamikia Mungu kuwa Yuda hakutekeleza ujumbe aliopewa. Anauliza, hadi lini Yuda waendelee katika uovu bila kuadhibiwa. Mungu anajibu kuwa anaandaa adhabu itakayotolewa kwa kutumia Wakaldayo (Wababeli). Habakuki anabisha mpango huo akisema: kama Mungu ni Mtakatifu na wa haki, na Wayahudi ni watu wake itawezekanaje Wakaldayo wenye maovu mengi kuliko Wayuda watumiwe na Mungu? Jibu la Mungu ni kuwa kila dhambi huleta hukumu. Hivyo wote watapata adhabu ya uovu wao.Habakuki, ambaye maana yake ni “kumbatia” au “mshindani mweleka” haelezi maisha yake binafsi na hataji kwa uwazi mwaka alipotoa ujumbe. Ujumbe wenyewe unaelekeza kuwa ni wakati Wakaldayo (Wababeli) walipokuwa wakitawala Ashuru, Misri na Yuda lakini kabla ya kubomoa Yerusalemu.Ujumbe wa Habakuki ni BWANA Mungu sio Mungu wa Israeli na Yuda tu, yeye ni Mungu wa ulimwengu wote. Yuda na Ukaldayo (Babeli) wataadhibiwa kwa kufuata maovu yao. Vile vile amtegemeaye Mungu akawa mwadilifu hana haja ya kuogopa hukumu maana “Mwenye haki ataishi kwa Imani”. Mungu atampa ushindi (2:4).Yaliyomo:1. Malalamiko ya Habakuki na Jibu la Mungu, Sura 1:1–2:52. Uovu wa Wababeli, Sura 2:6-203. Sala ya Habakuki, Sura 3
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help