Zaburi 103 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Shukrani kwa wema wa MunguYa Daudi.

1Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.

Naam, vyote vilivyo ndani yangu

Vilihimidi jina lake takatifu.

2Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA,

Wala usizisahau fadhili zake zote.

3 Isa 33:24; Mt 9:2; Mk 2:5; Lk 7:47; Kut 15:26; Yer 17:14 Akusamehe maovu yako yote,

Akuponya magonjwa yako yote,

4Aukomboa uhai wako na kaburi,

Akutia taji la fadhili na rehema,

5Aushibisha mema uzee wako,

Ujana wako ukarejezwa kama tai;

6BWANA ndiye afanyaye mambo ya haki,

Na hukumu kwa wote wanaoonewa.

7Alimjulisha Musa njia zake,

Wana wa Israeli matendo yake.

8 Kut 34:6; Hes 14:18; Kum 5:10; Yak 5:11 BWANA amejaa huruma na neema,

Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.

9 Isa 57:16; Yer 3:5; Mik 7:18 Yeye hatashutumu daima,

Wala hatashika hasira yake milele.

10 Ezr 9:13 Hakututenda kulingana na hatia zetu,

Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.

11Maana, kama mbingu zilivyoinuka juu ya nchi,

Ndivyo fadhili zake zilivyo kuu kwa wamchao.

12 Isa 43:25; Efe 1:7 Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,

Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.

13 Kum 8:5; Isa 63:15,16; Mal 3:17 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake,

Ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao.

14Kwa maana Yeye anatujua umbo letu,

Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi.

15Mwanadamu siku zake zi kama majani;

Kama ua la kondeni ndivyo anavyostawi.

16Maana upepo hupita juu yake, na kutoweka!

Lisionekane mahali lilipokuwa tena.

17 Kut 20:6 Bali fadhili za BWANA ni kwa wamchao

Tangu milele hata milele,

Na haki yake ni kwa vizazi vyote;

18 Kum 7:9 Kwa wale walishikao agano lake,

Na kuyakumbuka maagizo yake ili wayafanye.

19 Zab 47:2 BWANA ameweka kiti chake cha enzi mbinguni,

Na ufalme wake unavitawala vitu vyote.

20 Mt 6:10 Mhimidini BWANA, enyi malaika zake,

Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake,

Mkiisikiliza sauti ya neno lake.

21 Mwa 32:2; Dan 7:9 Mhimidini BWANA, enyi majeshi yake yote,

Ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake.

22Mhimidini BWANA, enyi matendo yake yote,

Mahali pote pa milki yake.

Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help