Yohana 14 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Yesu ni njia ya kwenda kwa Baba

1 Yn 14:27; Mk 11:22 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.

2Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.

3Yn 12:26; 17:24 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo.

4Nami niendako mwaijua njia.

5Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi tunaijuaje njia?

6Ebr 10:20; Mt 11:27; Yn 11:25; Rum 5:1,2 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

7Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.

8Filipo akamwambia, Bwana, utuoneshe Baba, yatutosha.

9Yn 12:45; Ebr 1:3; Mt 17:17 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuoneshe Baba?

10Yn 12:49 Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.

11Yn 14:20; 10:25,38 Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.

12Mk 16:19,20 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.

13Yn 15:7; Mk 11:24; 1 Yoh 5:14 Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.

14Yn 16:23,24 Mkiniomba neno lolote kwa jina langu, nitalifanya.

Ahadi ya kupewa Roho Mtakatifu

15 Yn 15:10; 1 Yoh 5:3 Mkinipenda, mtazishika amri zangu.

16Yn 14:26; 15:26; 16:7; 1 Yoh 2:1 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;

17Yn 7:39; 16:13; Mt 10:20; Rum 8:26 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.

18Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.

19Yn 16:16 Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai.

20Yn 17:21-23 Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.

212 Kor 3:18; 1 Yoh 5:3 Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.

22Mdo 10:41 Yuda (siye Iskarioti), akamwambia, Bwana, imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu?

23Yn 13:34; 14:21; Mit 8:17; Mt 18:20; 28:20; Efe 3:17; 2 Kor 6:16 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.

24Yn 7:16; 1 Yoh 2:5 Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenituma.

25Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu.

26Yn 14:16; Mt 10:19 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

27Yn 1:16,33; Flp 4:7 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.

28Yn 14:3,6,18; Lk 24:52 Mlisikia ya kwamba mimi niliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.

29Yn 13:19 Na sasa nimewaambia kabla halijatokea, ili litakapotokea mpate kuamini.

30Yn 12:31; Efe 2:2 Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana anakuja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.

31Yn 10:18; Mt 26:46; Mk 14:42 Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help