1 kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma.
262 Fal 2:2; Mwa 20:6; Rum 12:19; 2 Sam 18:32 Basi sasa, bwana wangu, aishivyo BWANA, na iishivyo nafsi yako, kwa kuwa BWANA amekuzuia usimwage damu, tena usijilipize kisasi mkono wako mwenyewe, basi sasa adui zako, na hao wamtakiao bwana wangu mabaya, wawe kama Nabali.
27Mwa 33:11 Na sasa zawadi hii, mjakazi wako aliyomletea bwana wangu, na wapewe vijana wamfuatao bwana wangu.
282 Sam 7:11; 1 Fal 9:5; 1 Nya 17:16; 1 Sam 24:11 Nakuomba ulisamehe kosa lake mjakazi wako, kwa kuwa hakika BWANA atamfanyia bwana wangu nyumba iliyo imara, kwa sababu bwana wangu anavipiga vita vya BWANA; tena uovu hautaonekana ndani yako siku zako zote.
29Kum 33:29; Zab 66:9; Mt 10:29,30; Mdo 17:28; Yer 10:18 Na hata ijapokuwa binadamu angeinuka akuwinde, na kuitafuta nafsi yako, hiyo nafsi ya bwana wangu itafungwa katika furushi la uhai pamoja na BWANA, Mungu wako; na nafsi za adui zako ndizo atakazozitupa nje, kama kutoka kati ya kombeo.
30Tena itakuwa, hapo BWANA atakapokuwa amemtendea bwana wangu sawasawa na mema yote aliyoyanena juu yako, na kukutawaza juu ya Israeli;
31hili halitakuwa kikwazo, wala chukizo la moyoni kwa bwana wangu, ama ya kuwa umemwaga damu bure, ama ya kuwa bwana wangu amejilipiza kisasi mwenyewe; tena hapo BWANA atakapokuwa amemtendea bwana wangu mema, ndipo umkumbuke mjakazi wako.
32Mwa 24:27; Kut 18:10; Ezr 7:27; Zab 41:12,13; 72:18; Lk 1:68; 2 Kor 8:16 Naye Daudi akamwambia Abigaili, Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye amekuleta hivi leo kunilaki;
33na ibarikiwe busara yako, na ubarikiwe wewe, uliyenizuia hivi leo nisimwage damu, wala kujilipiza kisasi kwa mkono wangu mwenyewe.
34Kwa kuwa ni kweli, aishivyo BWANA, Mungu wa Israeli, aliyenizuia nisikudhuru, kwamba usingalifanya haraka kuja kunilaki, hakika huyu Nabali asingaliachiwa hata mtoto mmoja wa kiume, kutakapopambazuka.
351 Sam 20:42; 2 Sam 15:9; 2 Fal 5:19; Lk 7:50; Mwa 19:21 Basi Daudi akapokea mkononi mwake vitu vile alivyomletea; akamwambia, Haya! Kwea kwa amani kwenda nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako, nami nimelikubali ombi lako.
36 2 Sam 13:23; Mit 20:1; 23:29; Isa 5:11; 28:1-3; Hos 4:11; Lk 21:34; Efe 5:18 Kisha Abigaili alimjia Nabali; na tazama, alikuwa amefanya karamu nyumbani mwake, kama karamu ya kifalme; na moyo wake huyo Nabali ukafurahiwa ndani yake, kwa maana amelewa kabisa. Kwa sababu hiyo hakumwambia neno, dogo wala kubwa, hadi kulipopambazuka.
37Kum 28:28; Ayu 15:21 Ikawa asubuhi, divai ilipokuwa imemtoka Nabali, mkewe alimwambia mambo hayo, na moyo wake ukafa ndani yake, akawa kama jiwe.
38Kut 12:29; 2 Sam 6:7; Ayu 12:10; 34:14,15; Zab 104:29; Mdo 12:23 Tena ikawa, yapata siku kumi baadaye, BWANA alimpiga huyo Nabali, hadi akafa.
39Mit 22:23; 2 Sam 3:28,29; 1 Fal 2:44; Est 7:10; Zab 7:16 Naye Daudi aliposikia ya kwamba Nabali amekufa, alisema, Na ahimidiwe BWANA ambaye amenitetea teto la shutumu langu mkononi mwa Nabali, na kumzuia mtumishi wake asitende maovu; tena uovu wake Nabali BWANA amemrudishia juu ya kichwa chake mwenyewe. Kisha Daudi akatuma watu, akamposa Abigaili ili amwoe.
40Na hao watumishi wa Daudi walipomjia huyo Abigaili huko Karmeli, walimwambia, wakasema, Daudi ametutuma kwako ili tukutwae uwe mkewe.
41Rut 2:10,13; Mit 15:33; 18:12 Naye akainuka na kujiinamisha kifudifudi mpaka chini, akasema, Tazama, mjakazi wako ni mtumishi wa kuwaosha miguu watumishi wa bwana wangu.
42Abigaili akafanya haraka, akainuka, akapanda punda, pamoja na vijakazi wake watano waliofuatana naye, akawafuata hao wajumbe wa Daudi, akawa mkewe.
43Yos 15:56; 2 Sam 3:2; Mwa 2:24; 1 Sam 30:5; Mt 19:5,8 Tena Daudi akamwoa Ahinoamu wa Yezreeli; wote wawili wakawa wake zake.
442 Sam 3:14-16; Isa 10:30 Lakini Sauli alikuwa amemposa Mikali, binti yake aliyekuwa mkewe Daudi, kwa Palti, mwana wa Laisha aliyekuwa mtu wa Galimu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.