Yeremia 47 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Hukumu juu ya Wafilisti

1 Isa 14:29-31; Eze 25:15-17; Yoe 3:4-8; Amo 1:6-8; Sef 2:4-7; Zek 9:5-7 Neno la BWANA lililomjia Yeremia, nabii, kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajashambulia Gaza.

2 Isa 8:7; Yer 1:14 BWANA asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi wataomboleza.

3Nah 3:2 Kwa sababu ya kishindo cha kukanyaga kwa kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbio mbio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya mngurumo wa magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu;

4Yer 25:22; Yoe 3:4; Amo 1:9,10; 9:7; Mwa 10:14 kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana BWANA atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori.

5 Sef 2:4 Upaa umeupata Gaza;

Ashkeloni umenyamazishwa

Mabaki ya bonde lao;

Hata lini utajikatakata?

6 Eze 21:3 Ee upanga wa BWANA,

Siku ngapi zitapita kabla hujatulia?

Ujitie katika ala yako;

Pumzika, utulie.

7 1 Sam 3:12; Mik 6:9 Utawezaje kutulia,

Ikiwa BWANA amekupa agizo?

Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani,

Ndipo alipoyaamuru hayo.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help