Hesabu UTANGULIZI - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

UTANGULIZIHesabu ni kitabu cha nne katika mfuatano wa vitabu vya Biblia. Jina Hesabu linatokana na sehemu mbili za kitabu hiki ambazo zinahusu hesabu mbili zilizofanywa kwa ajili ya jeshi. Hesabu ya kwanza ni kwa Waisraeli waliotoka Misri (1:1–2:32) na ya pili ni kwa kizazi kipya cha walioingia Nchi ya Ahadi (26:1-15).Kitabu hiki kinasimulia jinsi Waisraeli walivyopangwa katika makundi kwa kuzunguka Hema Takatifu, walivyosafiri toka Sinai kuelekea Kadesh-barnea na jinsi walivyojaribu kuingia katika Nchi ya Ahadi kutokea kusini lakini bila kufaulu. Aidha kuna masimulizi kuhusu imani, matumaini na moyo wa ushujaa kadhalika kutokuwa na imani, kukata tamaa, mashaka, woga na manung'uniko. Mungu ni mwaminifu kwa Agano na mwenye rehema. Masimulizi ya matukio ya kipindi chao cha kukaa jangwani miaka 38 wakijitayarisha na mwishoni walivyofanikiwa kutwaa sehemu za kusini mwa Mto Yordani na kuingia katika nchi waliyoahidiwa yana sehemu kubwa katika kitabu hiki.Yaliyomo:1. Hesabu ya kwanza na kazi ya Walawi, Sura 1–42. Sheria na maongozi, Sura 5–83. Pasaka ya pili na safari toka Sinai, Sura, 9–104. Uasi jangwani na sheria mbalimbali, Sura 11–195. Safari toka Kadeshi hadi Moabu, Sura 20–256. Hesabu ya pili na sheria kuhusu urithi, kafara na viapo, Sura 26–307. Katika Midiani na kugawana nchi, Sura 31–36
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help