1 Mk 11:1-10; Lk 19:29-38; Yn 12:12-19 Walipokaribia Yerusalemu, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu alipotuma wanafunzi wawili akiwaambia,
2Nendeni katika kijiji kile kinachowakabili, na mara mtaona punda amefungwa, na mwanapunda pamoja naye; wafungueni mniletee.
3Mt 26:18 Na kama mtu akiwaambia neno, semeni, Bwana anawahitaji; naye atawatuma mara moja.
4Haya yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema,
5 Zek 9:9; Isa 62:11 Mwambieni binti Sayuni
Tazama, mfalme wako anakuja kwako,
Mpole, naye amepanda punda,
Na mwanapunda, mtoto wa punda.
6Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya kama Yesu alivyowaamuru,
7wakamleta yule punda na mwanapunda, wakaweka nguo zao juu yao, naye akaketi juu yake.
82 Fal 9:13 Watu wengi katika ule mkutano wakatandaza nguo zao njiani; na wengine wakakata matawi ya miti, wakayatandaza njiani.
9Zab 118:25-26; 2 Sam 14:4 Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni.
10Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu?
11Mt 21:46 Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.
Yesu Atakasa hekalu12 Mk 11:11-24; Lk 19:45-48; Yn 2:14-16 Yesu akaingia ndani ya hekalu, akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa;
13Isa 56:7; Yer 7:11 akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.
14Na vipofu na viwete wakamwendea mle hekaluni, akawaponya.
15Zab 118:25 Lakini wakuu wa makuhani na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto waliopaza sauti zao hekaluni, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi! Walikasirika,
16Zab 8:3 wakamwambia, Wasikia hawa wasemavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umejiandalia sifa?
17Akawaacha, akatoka nje ya mji mpaka Bethania, akalala huko.
Yesu Aulaani Mtini18Na asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa.
19Lk 13:6 Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara.
20Wanafunzi walipoona, walistaajabu, wakisema, Jinsi gani mtini umenyauka mara?
21Mt 17:20; 1 Kor 13:2 Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng'oka, ukatupwe baharini, litatendeka.
22Na yoyote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea.
Swali kuhusu Mamlaka ya Yesu23 Mk 11:27-33; Lk 20:1-8 Na alipokwisha kuingia hekaluni, wakuu wa makuhani na wazee wa watu wakamwendea alipokuwa akifundisha, wakasema, Ni kwa amri gani unatenda mambo haya? Naye ni nani aliyekupa amri hii?Yn 2:18
24Yesu akajibu akawaambia, Na mimi nitawauliza neno moja; ambalo mkinijibu, nami nitawaambia ni kwa amri gani ninatenda haya.
25Ubatizo wa Yohana ulitoka wapi? Ulitoka mbinguni, au kwa wanadamu? Wakahojiana wao kwa wao, wakisema, Tukisema, Ulitoka mbinguni, atatuambia, Mbona basi hamkumwamini?
26Mt 14:5 Na tukisema, Ulitoka kwa wanadamu, twaogopa mkutano; maana watu wote wamwona Yohana kuwa ni nabii.
27Wakamjibu Yesu wakasema, Hatujui. Naye akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani ninatenda haya.
Mfano kuhusu Wana Wawili28Lakini mnaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda ukafanye kazi katika shamba la mizabibu.
29Mt 7:21 Naye akajibu akasema, Siendi, lakini baadaye akatubu akaenda.
30Akamwendea yule wa pili, akamwambia vile vile. Naye akajibu akasema, Naenda Bwana; lakini hakuenda.
31Lk 18:14 Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa kwanza. Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.
32Lk 3:12; 7:29-30 Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini.
Mfano wa Wakulima Waovu33 Mk 12:1-12; Lk 20:9-19 Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye shamba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungushia ua, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.Isa 5:1-2; Mt 25:14
34Wakati wa kuvuna matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake.
35Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe.
36Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza wakawatenda vile vile.
37Mwishowe akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu.
38Mt 27:18 Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake.
39Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua.
40Basi atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu, atawatendaje wale wakulima?
41Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake.
42Zab 118:22-23; Mdo 4:11; Rum 9:33; 1 Pet 2:6-8 Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko,
Jiwe walilolikataa waashi,
Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni;
Neno hili limetoka kwa Bwana,
Nalo ni la ajabu machoni petu?
43Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.
44Dan 2:34,35,44,45 Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika vipande vipande; naye yeyote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki.
45Wakuu wa makuhani na Mafarisayo, waliposikia mifano yake, walitambua ya kuwa anawanenea wao.
46Nao walipotafuta kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa maana wao walimwona kuwa nabii.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.