1 1 Yoh 4:15,16; 1 Pet 1:22,23 Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye.
2Katika hili tunajua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.
3Yn 14:15,23,24; Mt 11:30 Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
4Yn 16:33 Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.
51 Yoh 4:4 Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?
Ushuhuda kuhusu Mwana wa Mungu6 Yn 19:34,35 Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu.
7Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli.
8Kwa maana wako watatu washuhudiao, Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe.
10Rum 8:16; 1 Kor 15:15 Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.
11Yn 3:36 Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.
12Yn 3:36 Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.
Hitimisho13 Yn 20:31 Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu.
141 Yoh 3:21,22; Yn 14:13; 16:23 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.
15Na kama tukijua kwamba atusikia, tunapoomba chochote, tunajua kwamba tumetimiziwa zile haja tulizomwomba.
16Mt 12:31; Ebr 6:4-6 Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.
17Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.
18 1 Yoh 3:9; Yn 17:15 Tunajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi.
19Gal 1:4; Yn 8:47 Tunajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu.
20Yn 17:3; Rum 9:5 Nasi tunajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.
211 Kor 10:14 Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.