Wimbo ulio Bora 1 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

1 1 Fal 4:32 Wimbo ulio bora, wa Sulemani.

Mazungumzo ya bibi harusi na marafiki

2Kubusu na anibusu kwa kinywa chake.

Maana pendo lako lapita divai;

3 Wim 6:8; Mt 25:1; 2 Kor 11:2 Manukato yako yanukia vizuri;

Jina lako ni kama marhamu iliyomiminwa;

Kwa hiyo wanawali hukupenda.

4 Yer 31:3; Hos 11:4; Yn 6:44; Flp 3:12; Zab 45:14; Yn 14:2; Efe 2:6 Nivute nyuma yako, na tukimbie;

Mfalme ameniingiza vyumbani mwake.

Tutafurahi na kukushangilia;

Tutalinena pendo lako kuliko divai;

Ndiyo, ina haki wakupende.

5Mimi ni mweusi mweusi, lakini napendeza,

Enyi binti za Yerusalemu,

Mfano wa hema za Kedari,

Kama mapazia yake Sulemani.

6Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi mweusi,

Kwa sababu jua limeniunguza.

Wana wa mamangu walinikasirikia,

Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu;

Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda.

7 Yn 10:27 Nijulishe, ee mpendwa wa nafsi yangu,

Ni wapi utakapolisha kundi lako,

Ni wapi utakapolilaza adhuhuri.

Kwa nini niwe kama aliyefungiwa shela,

Karibu na makundi ya wenzako?

8Usipojua, wewe uliye mzuri katika wanawake,

Shika njia uzifuate nyayo za kondoo,

Na kuwalisha wana-mbuzi wako

Karibu na hema za wachungaji.

Mazungumzo ya bwana harusi, marafiki na bibi harusi

9 Wim 2:2; 2 Nya 1:16 Mpenzi wangu, nimekulinganisha

Na farasi katika magari ya Farao.

10 Eze 16:11 Mashavu yako ni mazuri kwa mashada,

Shingo yako kwa mikufu ya vito.

11Tutakutengenezea mashada ya dhahabu,

Yenye vifungo vya fedha.

12Muda mfalme alipoketi juu ya kochi,

Nardo yangu ilitoa harufu yake.

13Mpendwa wangu ni kama mfuko wa manemane

Ukilazwa usiku maziwani mwangu.

14Mpendwa wangu ni kama kishada cha hina,

Katika mizabibu huko Engedi.

15 Wim 4:1 Tazama, u mzuri, mpenzi wangu,

U mzuri, macho yako ni kama ya hua.

16Tazama, u mzuri, mpendwa wangu,

Wapendeza, na kitanda chetu ni majani;

17Nguzo za nyumba yetu ni mierezi,

Na viguzo vyetu ni miberoshi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help