1 2 Fal 11:21; 12:1 Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala; akatawala miaka arobaini huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Sibia wa Beer-sheba.
22 Nya 25:2; 26:5 Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA siku zote za Yehoyada kuhani.
3Yehoyada akamwoza wake wawili, naye akazaa watoto wa kiume na wa kike.
4Ikawa baada ya haya, Yoashi alikuwa na nia ya kuitengeneza nyumba ya Mungu.
52 Fal 12:4; 2 Nya 29:3; 34:8 Akawakusanya makuhani na Walawi, akawaambia, Nendeni katika miji ya Yuda, mkakusanye fedha kutoka Israeli wote, ili kuitengeneza nyumba ya Mungu wenu mwaka kwa mwaka, mkafanye bidii kuliharakisha neno hili. Lakini Walawi hawakuliharakisha.
62 Fal 12:7; Kut 30:12-16; Hes 1:50; 17:7,8; Mdo 7:44 Mfalme akamwita Yehoyada mkuu wao, akamwambia, Mbona hukuwataka Walawi waitoze Yuda na Yerusalemu kodi ya Musa mtumishi wa BWANA, na ya kusanyiko la Israeli, kwa ajili ya hema ya ushuhuda?
72 Nya 21:17; 22:3,4; Zab 12:8; 2 Fal 12:4 Kwa kuwa wana wa Athalia, yule mwanamke mwovu, walikuwa wameibomoa nyumba ya Mungu; na vitakatifu vyote vya nyumba ya BWANA wamewapatia Mabaali.
82 Fal 12:9 Basi mfalme akaamuru, nao wakatengeneza kasha, wakaliweka nje langoni pa nyumba ya BWANA.
9Kut 36:6 Wakapiga mbiu katika Yuda na Yerusalemu, kumletea BWANA kodi aliyoiweka Musa mtumishi wa Mungu, juu ya Israeli jangwani.
10Wakafurahi wakuu wote na watu wote, wakaleta na kutia ndani ya kasha, hadi wakaisha.
112 Fal 12:10 Ikawa wakati walipoletewa kasha wasimamizi wa mfalme kwa mkono wa Walawi, nao wakaona ya kwamba kuna fedha nyingi, huja karani wa mfalme, na msimamizi wake kuhani mkuu, wakatoa yaliyomo kashani, kisha hulichukua kasha, na kulirudisha mahali pake. Ndivyo walivyofanya siku kwa siku, wakakusanya fedha tele.
12Na mfalme na Yehoyada waliwapa hao waliofanya kazi ya utumishi wa nyumba ya BWANA; nao wakawaajiri waashi na maseremala ili kuitengeza nyumba ya BWANA, na hao pia wafuao chuma na shaba ili kuitengeza nyumba ya BWANA.
13Neh 4:7 Hivyo mafundi wakafanya kazi yao, nao wakaimaliza, wakaisimamisha nyumba ya Mungu kama ilivyopasa, wakaifanya imara.
141 Fal 7:50; 2 Fal 12:13; Kut 29:38; Ebr 7:27; 1 Pet 1:18,19; Ufu 5:9 Nao walipomaliza, wakaleta mbele ya mfalme na Yehoyada fedha iliyobaki, na kwavyo vikafanywa vyombo vya nyumba ya BWANA, vyombo vya utumishi, navyo vya kutolea, na miiko, na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya BWANA, mara kwa mara, siku zote za Yehoyada.
15 Ayu 5:26 Lakini Yehoyada akawa mzee, mwenye siku nyingi, akafa; alipokufa alikuwa na umri wa miaka mia moja na thelathini.
161 Fal 2:10 Wakamzika katika mji wa Daudi kati ya wafalme, kwa sababu ametenda mema katika Israeli, na kwa Mungu, na katika nyumba yake.
17Mdo 20:29 Hata baada ya kufa kwake Yehoyada, wakuu wa Yuda wakamwendea mfalme, wakamsujudia. Naye mfalme akawasikiliza maneno yao.
181 Fal 14:23; Yos 22:20; Amu 5:8; 2 Sam 24:1; 2 Nya 19:2; 28:13; Hos 5:10 Wakaiacha nyumba ya BWANA, Mungu wa baba zao; wakatumikia Maashera na sanamu; ghadhabu ikawajia Yuda na Yerusalemu kwa sababu ya hiyo hatia yao.
192 Nya 36:15; Neh 9:26; Yer 7:25,26; 25:4; Lk 11:47-51 Hata hivyo akawatuma manabii, ili kuwarudisha kwa BWANA; nao wakawashuhudia; lakini hawakukubali kuwasikiliza.
202 Nya 15:1,2; Amu 6:34; Hes 14:41; 1 Sam 13:13,14; Kum 29:25,26; Yer 2:19 Na Roho ya Mungu ikamjia Zekaria, mwana wa Yehoyada, kuhani; naye akasimama mbele ya watu palikuwa juu, akawaambia, Mungu asema hivi, Kwa nini ninyi mnazivunja amri za BWANA, hata msiweze kufanikiwa? Kwa kuwa mmemwacha BWANA, yeye naye amewaacha ninyi.
21Mt 23:35; Mdo 7:58 Basi, wakafanya shauri juu yake, wakampiga kwa mawe kwa amri ya mfalme katika ua wa nyumba ya BWANA.
22Basi hivyo mfalme Yoashi hakuukumbuka wema, ambao Yehoyada, baba yake Zekaria, alimfanyia, bali alimwua mwanawe. Naye alipokufa, alisema, BWANA na ayaangalie haya, akayalipie kisasi.
Kifo cha Yoashi23 2 Fal 12:17 Ikawa mwisho wa mwaka, wakakwea juu yake jeshi la Washami; wakafika Yuda na Yerusalemu, wakawaangamiza wakuu wa watu wote miongoni mwa watu, wakamletea mfalme wa Dameski nyara zao zote.
24Law 26:8,25; Kum 32:30; Isa 30:17; Kum 28:25; Isa 10:5 Maana wakaja jeshi la Washami watu wachache; BWANA akatia mikononi mwao jeshi kubwa mno, kwa sababu wamemwacha BWANA, Mungu wa baba zao. Hivyo wakamfanyia Yoashi hukumu.
252 Fal 12:18,20; Zab 10:14 Hata walipoondoka kwake, (nao walimwacha ameshikwa sana na maradhi,) watumishi wake mwenyewe wakamfanyia fitina kwa ajili ya damu ya mwana wa Yehoyada kuhani, wakamwua kitandani pake, akafa; wakamzika mjini mwa Daudi, lakini hawakumzika katika makaburi ya wafalme.
26Na hawa ndio waliomfanyia fitina, Zabadi mwana wa Shimeathi mwanamke Mwamoni, na Yehozabadi mwana wa Shimrithi mwanamke Mmoabi.
27Basi kwa habari ya wanawe, na ukubwa wa mizigo aliolemewa, na majengo ya nyumba ya Mungu, tazama, hayo yameandikwa katika maelezo ya kitabu cha Wafalme. Na Amazia mwanawe akatawala mahali pake.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.