1
23 Ayu 5:9 Neno hili limetoka kwa BWANA,
Nalo ni ajabu machoni petu.
24 2 Kor 6:2 Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA,
Tutashangilia na kuifurahia.
25 Mt 21:9; Mk 11:9; Yn 12:13 Ee BWANA, utuokoe, twakusihi;
Ee BWANA, utufanikishe, twakusihi.
26 Zek 4:7; Mt 21:9; 23:39; Mk 11:9; Lk 13:35; 19:38; Yn 12:13 Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la BWANA;
Tumewabariki toka nyumbani mwa BWANA.
27 Est 8:16; Mik 7:9; Mal 4:2 BWANA ndiye aliye Mungu,
Naye ndiye aliyetupa nuru.
Ifungeni dhabihu kwa kamba
Pembeni mwa madhabahu.
28 Kut 15:2; Isa 25:1 Ndiwe Mungu wangu, nami nitakushukuru,
Ndiwe Mungu wangu, nami nitakutukuza.
29Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema,
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.