1 Basi mfalme Ahasuero alitoza kodi katika nchi na katika visiwa vya bahari.
2 Na matendo yake yote yenye nguvu na ya ushujaa, na habari zote za ukuu wake Mordekai ambao alipewa na mfalme, hazikuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Umedi na Uajemi?
3 Kwa maana Mordekai Myahudi akiwa wa pili wake mfalme Ahasuero, na mkuu wa Wayahudi, amependeza mbele ya jamii ya ndugu zake; ambaye aliwajali watu wake, na kuiangalia hali njema ya wazawa wao wote.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.