1Nayainua macho yangu niitazame milima,
Msaada wangu utatoka wapi?
2Msaada wangu hutoka kwa BWANA,
Aliyezifanya mbingu na nchi.
3 1 Sam 2:9; Isa 27:3 Hatauacha mguu wako usogezwe;
Akulindaye hatasinzia;
4Naam, hatasinzia wala hatalala,
Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5BWANA ndiye mlinzi wako;
BWANA ni uvuli katika mkono wako wa kulia.
6 Isa 49:10 Jua halitakupiga mchana,
Wala mwezi wakati wa usiku.
7 Ayu 5:19; Zab 91:9,10; Mit 12:21 BWANA atakulinda na mabaya yote,
Atakulinda nafsi yako.
8 Kum 28:6; Mit 2:8 BWANA atakulinda utokapo na uingiapo,
Tangu sasa na hata milele.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.