Mhubiri 11 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Thamani ya kuwa na bidii

1 Kum 15:10; Mit 11:18; Mt 10:42; 2 Kor 9:6 Tupa chakula chako juu ya maji;

Maana utakiona baada ya siku nyingi.

2 Zab 112:9; Lk 6:30; Mik 5:5; Efe 5:16 Uwagawie sehemu watu saba, hata wanane;

Maana hujui baa gani litakalokuwa juu ya nchi.

3Mawingu yakiwa yamejaa mvua,

Yataimimina juu ya nchi;

Na mti ukianguka kuelekea kusini, au kaskazini,

Paangukapo ule mti, papo hapo utalala.

4Mwenye kuuangalia upepo hatapanda;

Naye ayatazamaye mawingu hatavuna.

5 Yn 3:8 Kama vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mja mzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote.

6Asubuhi panda mbegu zako,

Wala jioni usiulegeze mkono wako.

Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa, kama ni hii au hii, au kama zote zitafaa sawasawa.

Ujana na uzee

7Kweli nuru ni tamu, tena ni jambo la kupendeza macho kutazama jua.

8Naam, mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie yote; lakini na azikumbuke siku zijazo za giza, kwa maana zitakuwa nyingi. Mambo yote yajayo ni ubatili.

9Kum 29:19; Zab 81:12; Mdo 14:16; Efe 2:2,3; Mhu 12:14; Rum 2:6 Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na kinachotamaniwa na macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.

102 Kor 7:1 Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uuondoe ubaya mwilini mwako; kwa maana ujana ni ubatili, na utu uzima pia.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help