Zaburi 139 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Mungu asiyeweza kukwepwaKwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Zaburi.

1 Yer 12:3; Ufu 2:23 Ee BWANA, umenichunguza na kunijua.

2 2 Fal 19:27; Mt 9:4; Yn 2:24 Wewe wajua kuketi kwangu na kusimama kwangu;

Umelifahamu wazo langu tokea mbali.

3Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu,

Umeelewa na njia zangu zote.

4 Ebr 4:13 Maana hamna neno katika ulimi wangu

Usilolijua kabisa, BWANA.

5Umenizingira nyuma na mbele,

Ukaniwekea mkono wako.

6Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi,

Hayadirikiki, siwezi kuyafikia.

7Niende wapi nijiepushe na roho yako?

Niende wapi niukimbie uso wako?

8 Mit 15:11 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko;

Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.

9Ningezitwaa mbawa za asubuhi,

Na kukaa pande za mwisho za bahari;

10Huko nako mkono wako utaniongoza,

Na mkono wako wa kuume utanishika.

11Kama nikisema, Hakika giza litanifunika,

Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku;

12Giza nalo halikufichi kitu,

Bali usiku huangaza kama mchana;

Giza na mwanga kwako ni sawasawa.

13Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu,

Uliniunga tumboni mwa mama yangu.

14Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa

Kwa njia ya ajabu ya kutisha.

Matendo yako ni ya ajabu,

Na nafsi yangu yajua sana,

15Mifupa yangu haikusitirika kwako,

Nilipoumbwa kwa siri,

Nilipoungwa kwa ustadi katika pande za chini za nchi;

16Macho yako yaliniona kabla sijakamilika;

Kitabuni mwako ziliandikwa zote pia,

Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.

17Mawazo yako ni mazito sana kwangu;

Ee Mungu; nayo ni makuu sana.

18Kama ningeyahesabu ni mengi kuliko mchanga;

Niamkapo ningali pamoja nawe.

19 Isa 11:4 Ee Mungu, laiti ungewaua waovu!

Na laiti watu wa damu wangetoka kwangu;

20 Ayu 21:14,15; Yud 1:15 Wale wanaokusema kwa ubaya,

na kutenda maovu juu ya jina lako bure.

21Je! BWANA nisiwachukie wanaokuchukia?

Nisiudhike nao watu wanaokuasi?

22Nawachukia kwa upeo wa chuki,

Wamekuwa adui kwangu.

23 Ayu 31:6 Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu,

Unijaribu, uyajue mawazo yangu;

24 Mt 7:14; Yn 14:6 Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu,

Ukaniongoze katika njia ya milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help