1 Wakorintho 5 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Uzinzi hulichafua kanisa

1 Kum 22:30; Law 18:7,8 Hakika habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.

2Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo.

3Kol 2:5 Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo.

4Mt 16:19; 18:18; 2 Kor 13:10 Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu;

51 Tim 1:20; 1 Pet 4:6 kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.

6Gal 5:9 Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima?

7Kut 12:5,21; 13:7; Isa 53:7; 1 Pet 1:19 Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;

8Kut 13:7; 12:3-20; Kum 16:3 basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.

Uzinzi hauna budi kuhukumiwa

9 Mt 18:17; 2 The 3:14 Niliwaandikia katika barua yangu, kwamba msichangamane na wazinzi.

10Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.

112 The 3:6; Tit 3:10; 2 Yoh 1:10 Lakini, mambo yalivyo, niliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.

12Mk 4:11 Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamuwahukumu hao walio ndani?

13Kum 13:5; 17:7; 22:24 Lakini hao walio nje Mungu atawahukumu. Ninyi mwondoeni yule mbaya miongoni mwenu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help