Mathayo 15 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Mapokeo ya wazee

1 Mk 7:1-23 Ndipo Mafarisayo na waandishi toka Yerusalemu walipomwendea Yesu wakisema,

2Kum 4:2; Lk 11:38 Mbona wanafunzi wako huyavunja mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula.

3Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huivunja amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?

4Kut 20:12; 21:17; Kum 5:16; Law 20:9 Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe.

5Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, chochote kikupasacho nikusaidie kwacho nakitoa wakfu,

6basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.

7Isa 29:13 Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema,

8 Isa 29:13 Watu hawa huniheshimu kwa midomo;

Ila mioyo yao iko mbali nami.

9Nao waniabudu bure,

Wakifundisha mafundisho

Yaliyo maagizo ya wanadamu.

Mambo yatiayo unajisi

10Akawaita makutano akawaambia

11Mt 12:34; 1 Tim 4:4 Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi.

12Ndipo wanafunzi wake walipomwendea, wakamwambia, Wajua ya kuwa Mafarisayo walipolisikia neno lile walichukizwa?

13Yn 15:2 Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa.

14Lk 6:39; Mt 23:24; Yn 9:40; Rum 2:19 Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.

15Basi Petro akajibu, akamwambia, Tueleze mfano huo.

16Yesu akasema, Hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili?

17Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?

18Mt 12:34 Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.

19Mwa 8:21 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wizi, ushuhuda wa uongo, na matukano;

20hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi.

Imani ya mwanamke Mkanaani

21 Mk 7:24-30 Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni.

22Na tazama, mwanamke Mkanaani wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.

23Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa kuwa anaendelea kutupigia makelele nyuma yetu.

24Mt 10:6 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

25Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.

26Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.

27Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.

28Mt 8:10,13 Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.

Yesu awaponya watu wengi

29 Mk 7:31 Yesu akaondoka huko, akafika kando ya bahari ya Galilaya; akapanda mlimani, akaketi huko.

30Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu, mabubu, vilema, na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; akawaponya;

31Mk 7:37 hata ule mkutano wakastaajabu, walipowaona mabubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.

Kulishwa kwa watu elfu nne

32 Mk 8:1-10 Yesu akawaita wanafunzi wake, akasema, Nawahurumia mkutano, kwa kuwa yapata siku tatu wamekaa pamoja nami, wala hawana kitu cha kula, tena sitaki kuwaaga wakiwa na njaa, wasije wakazimia njiani.Mt 14:14

33Wanafunzi wake wakamwambia, Tupate wapi mikate mingi hapa nyikani, hata kushibisha mkutano mkuu namna hii?

34Yesu akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba, na visamaki vichache.

35Akawaagiza mkutano waketi chini;

36akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano.

37Wakala wote wakashiba; wakayaokota mabaki ya vipande vya mikate makanda saba, yamejaa.

38Nao waliokula walikuwa wanaume elfu nne, bila kuhesabu wanawake na watoto.

39Akawaaga makutano, akapanda katika mashua, akaenda pande za Magadani.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help