2Samweli 2 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Daudi atiwa mafuta kuwa mfalme wa Yuda

1 mwana wa Sauli, alikuwa na umri wa miaka arobaini alipoanza kutawala juu ya Israeli, akatawala miaka miwili.) Lakini nyumba ya Yuda waliandamana na Daudi.

11Na wakati Daudi alipotawala Hebroni juu ya nyumba ya Yuda ilikuwa miaka saba na miezi sita.

Vita vya Gibeoni

12 napo ni katika Gibeoni.

171 Fal 20:11 Vita vile vilikuwa vikali sana siku ile; naye Abneri akashindwa, na watu wa Israeli, mbele ya watumishi wa Daudi.

181 Nya 2:16; 12:8; Zab 18:33; Wim 2:17; 8:14 Na wana watatu wa Seruya walikuwako huko, Yoabu, na Abishai, na Asaheli; na Asaheli alikuwa mwepesi wa miguu kama kulungu.

19Naye Asaheli akamfuatia Abneri; na katika kwenda kwake hakugeuka kwenda mkono wa kulia wala mkono wa kushoto katika kumfuatia Abneri.

20Basi Abneri akatazama nyuma yake, akasema, Ni wewe, Asaheli? Akajibu, Ni mimi.

211 Sam 17:42 Basi Abneri akamwambia, Geuka mkono wa kulia au mkono wa kushoto, ukamshike mmoja wa vijana, ukazitwae silaha zake. Lakini Asaheli hakukubali kugeuka na kuacha kumfuata.

22Abneri akamwambia Asaheli mara ya pili, Geuka, acha kunifuatia mimi; kwa nini nikupige hadi chini? Hapo ningewezaje kuinua uso wangu mbele ya Yoabu, ndugu yako?

232 Sam 3:27; 4:6 Lakini akakataa kugeuka; kwa hiyo Abneri akampiga tumboni kwa ncha ya nyuma ya mkuki wake, ule mkuki ukamtoka kwa nyuma; naye akaanguka hapo, akafa papo hapo; ikawa, watu wote waliofika hapo, alipoanguka Asaheli na kufa, wakasimama.

24Yos 9:3; 10:2 Ila Yoabu na Abishai wakamfuatia Abneri; na jua likachwa hapo walipoufikia mlima wa Ama, uelekeao Gia, katika njia ya nyika ya Gibeoni.

25Nao wana wa Benyamini wakakusanyika pamoja nyuma ya Abneri, wakawa kikosi kimoja, wakasimama juu ya mlima.

26Ayu 18:2; 19:2; Zab 4:2; Mdo 7:26 Ndipo huyo Abneri akamwita Yoabu, akasema, Je! Upanga uwale watu siku zote? Je! Hujui ya kwamba utakuwa uchungu mwisho wake? Basi itakuwa hata lini usijewaamuru watu warudi na kuacha kuwafuatia ndugu zao?

27Mit 17:14; 20:18; Lk 14:31,32 Naye Yoabu akasema, Aishivyo Mungu, usingalinena, basi asubuhi wangalikwenda zao, wasiwafuatie kila mtu ndugu yake.

28Basi Yoabu akapiga tarumbeta, na watu wote wakasimama, wasiwafuatie Israeli tena, wala hawakupigana tena.

29Wim 2:17; Mwa 32:2; Yos 21:38; 2 Sam 17:24 Wakaenda Abneri na watu wake usiku ule wote kati ya ile Araba; wakavuka Yordani, wakapita kati ya Bithroni yote, wakaja Mahanaimu.

30Akarudi Yoabu naye kutoka kumfuatia Abneri; na alipokwisha kuwakusanya watu wote pamoja, wa hao watumishi wa Daudi walipungukiwa na watu kumi na tisa pamoja na Asaheli.

31Ila watumishi wa Daudi walikuwa wamewapiga watu wa Benyamini, na watu wa Abneri, hata wakafa watu mia tatu na sitini.

32Mwa 47:29,30; 49:29; Amu 8:32; 2 Sam 17:23; 19:37 Nao wakamchukua Asaheli, wakamzika katika kaburi la baba yake, lililokuwako Bethlehemu. Yoabu na watu wake wakaenda usiku kucha, wakapambazukiwa huko Hebroni.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help