1BWANA asipoijenga nyumba
Waijengao wanafanya kazi bure.
BWANA asipoulinda mji
Yeye aulindaye anakesha bure.
2 Mwa 3:17 Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema,
Na kukawia kwenda kulala,
Na kula chakula cha taabu;
Yeye humpa mpenzi wake usingizi.
3 Mwa 33:5; Kum 28:4 Tazama, watoto ni urithi kutoka kwa BWANA,
Uzao wa tumbo ni thawabu.
4Kama mishale mkononi mwa shujaa,
Ndivyo walivyo watoto wa ujanani.
5Heri mtu yule
Aliyelijaza podo lake hivyo.
Naam, hawataona aibu
Wanaposema na adui langoni.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.