Zaburi 74 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Ombi la kutaka msaada wakati wa kushindwaUtenzi wa Asafu.

1 Zab 95:7; Yer 23:1; Eze 34:8,31; Lk 12:32 Ee Mungu, mbona umetutupa milele?

Kwa nini hasira yako inatoka moshi

Juu ya kondoo wa malisho yako?

2Ulikumbuke kusanyiko lako,

Ulilolinunua zamani.

Ulilolikomboa liwe kabila la urithi wako,

Mlima Sayuni ulioufanya maskani yako.

3Upite na kupaona palipoharibika milele;

Adui ameufanya kila ubaya katika patakatifu.

4 Dan 6:27 Watesi wako wamenguruma kati ya kusanyiko lako;

Wameweka bendera zao ziwe alama.

5Wanaonekana kama watu wainuao mashoka,

Waikate miti ya msituni.

6Na sasa nakishi yake yote pia

Wanaivunjavunja kwa mashoka na nyundo.

7Wamepatia moto patakatifu pako;

Wamelinajisi kao la jina lako hata chini.

8 Zab 83:4 Walisema mioyoni mwao,

Na tuwaangamize kabisa;

Mahali penye mikutano ya Mungu

Wamepachoma moto katika nchi pia.

9 1 Sam 3:1; Mik 3:6; Mt 16:4 Hatuzioni ishara zetu, wala sasa hakuna nabii,

Wala kwetu hakuna ajuaye, hadi lini?

10Ee Mungu, mtesi atalaumu hata lini?

Adui alidharau jina lako hata milele?

11Mbona unaurudisha mkono wako,

Naam, mkono wako wa kulia,

Uutoe kifuani mwako,

Ukawaangamize kabisa.

12 Zab 44:4 Lakini Mungu ni mfalme wangu tokea zamani,

Afanyaye mambo ya wokovu katikati ya nchi.

13 Kut 14:21; Isa 51:9 Wewe umeipasua bahari kwa nguvu zako,

Umevivunja vichwa vya nyangumi juu ya maji.

14 Kut 17:5,6; Hes 14:9; 20:11; Ayu 41:1; Isa 11:16; 27:1; Yos 3:13; Zab 72:9; 104:26; 105:41; Hab 3:9; Ufu 16:12 Wewe ulivivunja vichwa vya Lewiathani,

Awe chakula cha watu wa jangwani.

15Wewe ulitokeza chemchemi na kijito;

Wewe ulikausha mito yenye maji siku zote.

16Mchana ni wako, usiku nao ni wako,

Ndiwe uliyeufanya mwanga na jua.

17 Mdo 17:26 Wewe uliiweka mipaka yote ya dunia,

Majira ya joto na ya baridi wewe uliyafanya.

18 Ufu 16:19 Ee BWANA, uyakumbuke hayo, adui amelaumu,

Na watu wapumbavu wamelidharau jina lako.

19 Wim 2:14; 4:1 Usimpe mnyama mkali uhai wa njiwa wako;

Usiwasahau milele watu wako walioonewa.

20 Mwa 17:7; Law 26:44; Yer 33:21 Ulitafakari agano lako;

Maana mahali kwenye giza katika nchi

Kumejaa makao ya ukatili.

21 Zab 9:18 Aliyeonewa asirejee ametiwa haya,

Mnyonge na mhitaji na walisifu jina lako.

22 Isa 37:23 Ee Mungu, usimame, ujitetee mwenyewe,

Ukumbuke unavyotukanwa na mpumbavu mchana kutwa.

23Usiisahau sauti ya watesi wako,

Ghasia yao wanaokupinga inapaa daima.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help