1 Wakorintho 15 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Kufufuka kwa Kristo

1Basi, ndugu zangu, nawaarifu ile Injili niliyowahubiria; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama,

2na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiria isipokuwa mliamini bure.

3Isa 53:5-12 Kwa maana niliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo Maandiko;

4Zab 16:8-10; Mt 12:40; Mdo 2:24-32; 2 Fal 20:5; Isa 54:7; Hos 6:2 na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo Maandiko;

5Mt 28:16-17; Mk 16:14; Lk 24:34,36; Yn 20:19 na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Kumi na Wawili;

6baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala;

7Lk 24:50 baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote;

8Mdo 9:3-6; 1 Kor 9:1 na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake.

9Mdo 8:3; Efe 3:8; Mt 5:19; 1 Tim 1:15 Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mtume, kwa sababu nililiudhi kanisa la Mungu.

102 Kor 11:5,23; 6:1 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nilizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.

11Basi kama ni mimi, au kama ni wao, ndivyo tuhubirivyo na ndivyo mlivyoamini.

Kufufuliwa kwa mwili

12Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu?

13Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka;

14tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure.

15Mdo 1:22; 5:32 Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.

161 Kor 6:14 Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka.

17Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu.

18Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea.

19Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote.

20 Kol 1:18; 1 Kor 11:30 Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala.

21Mwa 3:17-19; Rum 5:12,18 Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu.

22Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.

231 The 4:16; Ufu 20:5 Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja.

24Dan 2:44 Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.

25Zab 110:1; Mt 22:44 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke adui zake wote chini ya miguu yake.

26Ufu 20:14; 21:4 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.

27Zab 8:6 Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.

28Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.

29Au je! Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao?

30Rum 8:36 Na sisi, kwa nini tumo hatarini kila saa?

312 Kor 4:10,11 Naam, ndugu, kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu, ninakufa kila siku.

32Isa 22:13 Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nilipigana na hayawani wakali kule Efeso, nina faida gani? Wasipofufuliwa wafu, na tule, na tunywe, maana kesho tutakufa.

33Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.

34Rum 13:11; Efe 5:14; 1 Kor 6:5; Mdo 26:8 Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.

Mwili wa ufufuo

35Lakini labda mtu atasema, Wafu wafufuliwaje? Nao huja kwa mwili gani?

36Yn 12:24 Ewe mpumbavu! Uipandayo haihuiki, isipokufa;

37nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, ila chembe tupu, ikiwa ni ya ngano au nyingineyo;

38Mwa 1:11 lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na kila mbegu mwili wake.

39Nyama zote hazifanani; nyingine ni ya wanadamu, nyingine ya hayawani, nyingine ya ndege, nyingine ya samaki.

40Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali.

41Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota.

42Kadhalika na kiyama ya wafu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutoharibika;

43Flp 3:20,21 hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu;

44hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko.

45Mwa 2:7; Yn 6:63; 2 Kor 3:6,17 Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa kiumbe aliye hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha.

46Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho.

47Mwa 2:7 Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni.

48Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni.

49Mwa 5:3 Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni.

50 1 Kor 6:13 Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutoharibika.

511 The 4:15-17 Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,

52Mt 24:31; 1 The 4:16 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.

532 Kor 5:4 Maana sharti huu uharibikao uvae kutoharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.

54Isa 25:8 Basi huu uharibikao utakapovaa kutoharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa katika ushindi.

55Hos 13:14; Isa 25:8 Kuko wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? Uko wapi, Ewe mauti, uchungu wako?

56Rum 7:13; 6:14 Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.

57Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

582 Nya 15:7; Ufu 14:13 Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa mnajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help