1Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia,
2 kwa sababu ya hicho kishada walichokata huko wana wa Israeli.
Taarifa ya wapelelezi25Wakarejea baada ya kuipeleleza nchi, mwisho wa siku arobaini.
26Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote, wakawaonyesha matunda ya nchi.
27Kut 3:8; 13:5; 33:3; Kum 1:25 Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, kwa hakika, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, kwa uthibitisho, haya ndiyo matunda yake.
28Kum 1:28; 9:1,2 Lakini watu wanaokaa katika nchi ile ni wenye nguvu, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa sana; na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko.
29Kut 17:8; Amu 6:3; Hes 14:43; 1 Sam 14:48; 15:3; 30:1 Amaleki anakaa katika nchi ya Negebu; na Mhiti, na Myebusi, na Mwamori wanakaa katika milima, na Mkanaani anakaa karibu na bahari; na kando ya ukingo wa Yordani.
30Yos 14:7; Zab 60:12; 118:10; Isa 11:10; Rum 8:31; Flp 4:13; Ebr 11:33,34 Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara moja tukaimiliki; maana twaweza kushinda bila shaka.
31Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi.
32Mt 23:13; Amo 2:9 Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala wakazi wake; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu wakubwa mno.
33Mwa 6:4; 1 Sam 17:4-7; Isa 40:22 Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.