1 Mambo ya Nyakati 24 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Mgawanyo wa makuhani

1 Kut 6:23; Law 10:1; Hes 3:2; 26:60 Na zamu za wana wa Haruni ni hizi. Wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.

2Hes 3:4; 26:61 Lakini hao Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, wala hawakuwa na watoto; kwa hiyo Eleazari na Ithamari wakafanya ukuhani.

3Akawagawanya Daudi, na Sadoki wa wana wa Eleazari, na Ahimeleki wa wana wa Ithamari, katika utumishi kwa kadiri ya huduma yao.

4Wakaonekana wakuu wengi wa wana wa Eleazari kuliko wa wana wa Ithamari; wakagawanyika hivi; wa wana wa Eleazari kulikuwa na kumi na sita, waliokuwa wakuu wa koo za baba zao; na wa wana wa Ithamari, kulingana na koo za baba zao, wanane.

5Yos 18:10; Mit 16:33; 18:18; Mdo 1:26 Ndivyo walivyogawanyika kwa kura, wao kwa wao; kwani kulikuwa na wakuu wa patakatifu, na watumishi wa Mungu, wa wana wa Eleazari, na wa wana wa Ithamari pia.

61 Fal 4:3; Neh 8:4 Naye Shemaya, mwana wa Nethaneli, mwandishi, aliyekuwa wa Walawi, akawaandika mbele ya mfalme, na mbele ya wakuu, na Sadoki kuhani, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari, na wakuu wa koo za baba za makuhani, na za Walawi; ikatwaliwa ya Eleazari koo moja ya baba, na moja ikatwaliwa ya Ithamari.

7Ezr 2:36; Neh 7:39 Kura ya kwanza ikamtokea Yehoiaribu, na ya pili Yedaya;

8Ezr 10:21 ya tatu Harimu, ya nne Seorimu;

9ya tano Malkia, ya sita Miyamini;

10Neh 12:4,17; Lk 1:5 ya saba Hakosi, ya nane Abia;

11ya tisa Yeshua, ya kumi Shekania;

12ya kumi na moja Eliashibu, ya kumi na mbili Yakimu;

13ya kumi na tatu Hupa, ya kumi na nne Yeshebeabu;

14ya kumi na tano Bilga, ya kumi na sita Imeri;

15ya kumi na saba Heziri, ya kumi na nane Hapisesi;

16ya kumi na tisa Pethahia, ya ishirini Ezekieli;

17ya ishirini na moja Yakini, ya ishirini na mbili Gamuli;

18ya ishirini na tatu Delaya, ya ishirini na nne Maazia.

19Hes 4:49; 1 Nya 9:25; 2 Fal 5:7; Lk 1:8,23 Huu ndio utaratibu wa zamu zao katika huduma yao, ya kuingia nyumbani mwa BWANA kwa kadiri ya agizo lao, kwa mkono wa Haruni baba yao, kama BWANA, Mungu wa Israeli, alivyomwamuru.

Walawi wengineo

20 1 Nya 23:16 Na wa wana wa Lawi, waliosalia; wa wana wa Amramu, Shebueli; wa wana wa Shebueli, Yedeya.

211 Nya 23:17 Wa Rehabia; wa wana wa Rehabia, Ishia mkuu wao.

221 Nya 23:15 Wa Waishari, Shelomothi; wa wana wa Shelomothi, Yahathi.

231 Nya 15:9; 23:19 Na wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, Yekameamu wa nne.

24Wana wa Uzieli, Mika; wa wana wa Mika, Shamiri.

25Nduguye Mika, Ishia; wa wana wa Ishia, Zekaria.

26Kut 6:19; 1 Nya 23:21; Hes 3:20,33 Wana wa Merari; Mali na Mushi; wana wa Yaazia; Beno.

27Wana wa Merari; wa Yaazia; Beno, na Shohamu, na Zakuri, na Ibri.

281 Nya 23:22 Wa Mali; Eleazari, asiyekuwa na wana.

29Wa Kishi; wana wa Kishi; Yerameeli.

301 Nya 23:23 Na wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi. Hao ndio wana wa Walawi, kwa kufuata koo za baba zao.

31Hao nao wakapigiwa kura vile vile, kama ndugu zao wana wa Haruni, machoni pa Daudi mfalme, na Sadoki, na Ahimeleki, na wakuu wa koo za baba za makuhani na za Walawi; koo za baba za mkuu, vile vile kama za nduguye mdogo.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help