Zaburi 138 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Shukrani na sifa ya Daudi

1 Zab 119:46 Nitakushukuru kwa moyo wangu wote,

Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.

2 1 Fal 8:29; Zab 5:7; Dan 6:10; Yon 2:7; Isa 42:21 Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu,

Nitalishukuru jina lako,

Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako,

Kwa maana umeikuza ahadi yako,

na jina lako juu ya vyote.

3 2 Kor 12:9; Zek 10:12 Siku ile niliyokuita uliniitikia,

Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.

4Ee BWANA, wafalme wote wa dunia watakushukuru,

Watakapoyasikia maneno ya kinywa chako.

5Naam, wataziimba njia za BWANA,

Kwa maana utukufu wa BWANA ni mkuu.

6 Mit 3:34; Yak 4:6 Ingawa BWANA yuko juu, anamjali mnyenyekevu,

Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali.

7 Zab 23:3 Nijapopitia katika shida,

Unanilinda juu ya hasira ya adui zangu,

Unaunyosha mkono wako,

Na mkono wako wa kuume unaniokoa.

8 Zab 57:2; Flp 1:6 BWANA atanitimizia malengo yake kwangu;

Ee BWANA, fadhili zako ni za milele;

Usiiache kazi ya mikono yako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help