1 upepo uharibuo.
2 alivyotwaliwa!
Naye sifa ya dunia yote alivyoshambuliwa!
Jinsi Babeli alivyokuwa ukiwa
Katikati ya mataifa!
42 Isa 8:7,8 Bahari imefika juu ya Babeli,
Umefunikwa kwa wingi wa mawimbi yake.
43Miji yake imekuwa maganjo;
Nchi ya ukame, na jangwa;
Nchi asimokaa mtu yeyote,
Wala hapiti mwanadamu huko.
44 Yer 50:2 Nami nitafanya hukumu juu ya Beli katika Babeli, nami nitavitoa katika kinywa chake alivyovimeza; wala mataifa hawatamwendea tena; naam, ukuta wa Babeli utaanguka.
45 Ufu 18:4 Enyi watu wangu; tokeni katikati yake, mkajiokoe nafsi zenu kutoka na hasira kali ya BWANA, kila mmoja wenu.
462 Fal 19:7 Wala isizimie mioyo yenu, wala msiiogope habari itakayosikiwa katika nchi; maana habari itakuja mwaka mmoja, na baadaye mwaka wa pili habari itakuja, na udhalimu katika nchi, mwenye kutawala akishindana na mwenye kutawala.
47Isa 44:23; Yer 50:3 Basi angalia, siku zitakuja, ambazo katika siku hizo, nitafanya hukumu juu ya sanamu za Babeli, na nchi yake yote itatahayarika; na watu wake wote waliouawa wataanguka katikati yake.
48Ufu 18:20; Yer 44:28 Ndipo mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo, vitaimba kwa furaha juu ya Babeli; kwa maana watu waangamizao watamjia kutoka kaskazini, asema BWANA.
49Ufu 18:24 Kama vile Babeli alivyowaangusha watu wa Israeli waliouawa, ndivyo watakavyoanguka katika Babeli watu wa nchi yake nzima waliouawa.
50 Yer 44:28 Ninyi mliojiepusha na upanga,
Nendeni zenu, msisimame;
Mkumbukeni BWANA tokea mbali,
Na Yerusalemu ukatiwe mioyoni mwenu.
51 Zab 44:15 Twaona haya kwa kuwa tumesikia shutuma;
Fedheha imetufunika nyuso zetu;
Kwa sababu wageni wamepaingia
Patakatifu pa nyumba ya BWANA.
52Kwa sababu hiyo siku zinakuja, asema BWANA, nitakapozihukumu sanamu zake; na katika nchi yake yote waliojeruhiwa wataomboleza.
53Yer 49:16; Amo 9:2 Babeli ujapopanda mbinguni, na ujapopafanya mahali pa juu penye nguvu zake kuwa ngome, hata hivyo toka kwangu wenye kuangamiza watamwendea, asema BWANA.
54 Isa 13:6-9; 15:5; Yer 50:22; Sef 1:10 Sauti ya kilio kutoka Babeli,
Na ya uangamizi mkuu toka nchi ya Wakaldayo!
55Maana BWANA amwangamiza Babeli,
Na kuikomesha sauti kuu ndani yake;
Na mawimbi yake yavuma kama maji mengi,
Mshindo wa sauti zao wafanya makelele;
56 Kum 32:35; Zab 94:1 Kwa maana mwenye kuangamiza amefika kwake;
Naam, amefika Babeli;
Na mashujaa wake wametwaliwa;
Pinde zao zimevunjika kabisa;
Maana BWANA ni Mungu wa kisasi;
Hakika yake yeye atalipa.
57 Yer 46:18; 48:15 Nami nitawalevya wakuu wake, na watu wake wenye hekima, watawala wake, na makamanda wake, na mashujaa wake; nao watalala usingizi wa milele, wasiamke, asema Mfalme, BWANA wa majeshi, ambaye jina lake ni BWANA.
58Hab 2:13 BWANA wa majeshi asema hivi, Kuta pana za Babeli zitabomolewa kabisa, na malango yake marefu yatateketezwa; nao watu watajitaabisha kwa ubatili, na mataifa kwa moto; nao watachoka.
Yeremia amwamuru Seraya59Neno ambalo Yeremia, nabii, alimwamuru Seraya, mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, alipokwenda Babeli pamoja na Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne wa kumiliki kwake. Basi Seraya alikuwa msimamizi mkuu wa nyumba ya mfalme.
60Naye Yeremia akaandika katika kitabu kuhusu mabaya yote yatakayoupata Babeli, maneno hayo yote yaliyoandikwa juu ya Babeli.
61Naye Yeremia akamwambia Seraya, Utakapofika Babeli, basi angalia uyasome maneno haya yote,
62Yer 50:3,39 ukaseme, Ee BWANA, umenena kuhusu mji huu kwamba utakatiliwa mbali, usikaliwe na awaye yote, wala wanadamu wala wanyama, lakini uwe ukiwa hata milele.
63Ufu 18:21 Tena itakuwa utakapokwisha kukisoma kitabu hicho, utakifungia jiwe, na kukitupa katika mto Frati;
64nawe utasema, Hivyo ndivyo utakavyozama Babeli, wala hautazuka tena, kwa sababu ya mabaya yote nitakayoleta juu yake; nao watachoka.
Maneno ya Yeremia yamefika hata hapa.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.