1Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,
2Enzi na hofu zi pamoja na Mungu;
Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka.
3 Mwa 1:3-5,14-16; Zab 19:4-6; 139:8,11; Mt 5:45; Yak 1:17 Je! Majeshi yake yahesabika?
Ni nani asiyetokewa na mwanga wake?
4 Ayu 4:17; 9:2; Zab 130:3; 143:2; Rum 3:19,20 Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu?
Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke?
5Tazama, hata mwezi hauangazi,
Wala nyota si safi machoni pake;
6 Zab 22:6 Sembuse mtu, aliye mdudu!
Na mwanadamu, ambaye ni buu!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.