Zaburi 4 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Ombi la kuokolewa kutoka kwa aduiKwa mwimbishaji: kwa ala za muziki zenye nyuzi. Zaburi ya Daudi.

1Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo;

Uliniokoa nilipokuwa katika shida;

Unifadhili na kuisikia sala yangu.

2Enyi wanadamu, hadi lini utukufu wangu utafedheheka?

Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo hadi lini?

3 Kut 33:16; 2 Pet 2:9 Bali jueni ya kuwa BWANA amejiteulia mtauwa;

BWANA husikia nimwitapo.

4 Efe 4:26; Mit 3:7 Muwe na hofu wala msitende dhambi,

Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.

5 Kum 33:19; Zab 37:3 Toeni dhabihu za haki,

Na kumtumaini BWANA.

6 Zab 80:3 Wengi husema, Nani atakayetuonesha mema?

BWANA, utuinulie nuru ya uso wako.

7Umenitia furaha moyoni mwangu,

Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.

8 Law 26:5; Kum 12:10; Yn 14:27; Flp 4:7 Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara,

Maana Wewe, BWANA, peke yako,

Ndiwe unijaliaye kukaa salama.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help