1 rangi ya chanikiwiti, nawe utachora juu yake majina ya wana wa Israeli;
10majina yao sita katika kito kimoja, na majina sita yaliyosalia katika kile kito cha pili, kwa utaratibu wa kuzaliwa kwao.
11Kwa kazi ya mtu mwenye kuchora mawe kama vile mihuri ichorwavyo, utavichora hivi vito viwili, sawasawa na majina ya wana wa Israeli, nawe utavitia katika vijalizo vya dhahabu.
12 katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu; nazo zitakuwa juu ya moyo wa Haruni, hapo atakapoingia ndani mbele za BWANA; na Haruni atachukua hukumu ya hao wana wa Israeli juu ya moyo wake mbele za BWANA daima.
Mavazi mengine ya ukuhani31 ili lisipasuke.
33Nawe katika pindo zake utatia makomamanga ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, kuzunguka pindo zake kotekote; na njuga za dhahabu kati ya hayo makomamanga pande zote;
34njuga ya dhahabu na komamanga, katika pindo za joho kuizunguka pande zote.
35Nayo itakuwa juu ya Haruni akitumika; na sauti ya hizo njuga itasikika hapo aingiapo ndani ya mahali patakatifu mbele za BWANA na hapo atokapo nje, ili kwamba asife.
36 Kut 39:30; Law 8:9; 1 Nya 16:29; Zab 29:2; 93:5; Zek 14:20; Ebr 4:15; 7:26 Nawe fanya bamba la dhahabu safi na kuchora juu yake, mfano wa michoro ya mihuri, MTAKATIFU KWA BWANA.
37Nawe ulitie hilo bamba katika ukanda wa rangi ya buluu, nalo litakuwa katika kile kilemba; litakuwa upande wa mbele wa kile kilemba.
38Law 10:17; 22:9; Isa 53:11; Yn 1:29; Ebr 9:28; 1 Pet 2:24; Law 1:4; 23:11; Isa 56:7 Nalo litakuwa katika kipaji cha uso cha Haruni, na Haruni atauchukua uovu wa vile vitu vitakatifu, watakavyovitakasa hao wana wa Israeli katika vipawa vyao vyote vitakatifu, nalo litakuwa katika kipaji chake cha uso siku zote, ili vipate kukubaliwa mbele za BWANA.
39Na hiyo kanzu utaifuma ya kitani nzuri ya kazi ya urembo, ufanye na kilemba cha nguo ya kitani nzuri, nawe utafanya mshipi wenye kunakishiwa vizuri.
40 Kut 39:27; Eze 44:17,18 Kisha utafanya kanzu kwa ajili ya wana wa Haruni, nawe wafanyie mishipi, wafanyie na kofia kwa utukufu na uzuri.
41Kut 29:7; 30:30; Law 10:7 Nawe mvike huyo nduguyo Haruni na wanawe nao mavazi hayo; nawe watie mafuta, na kuwaweka kwa kazi takatifu, na kuwatakasa, ili wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani.
42Law 6:10; Eze 44:18 Nawe wafanyie suruali za nguo ya kitani, ili kufunika tupu ya miili yao; suruali hizo zitafika tangu kiunoni hadi mapajani;
43Kut 20:26; Law 20:19,20; Hes 18:22; Law 17:7 na Haruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania, au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike katika mahali patakatifu; wasije wakachukua uovu, wakafa; hii itakuwa ni amri ya milele kwake yeye, na kwa wazao wake.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.