1Rehema na hukumu nitaziimba,
Ee BWANA, nitakuimbia zaburi.
2 1 Sam 18:14; Mwa 18:19; Kum 6:7; 1 Fal 9:4 Nitaiangalia njia ya unyofu;
Utakuja kwangu lini?
Nitakwenda kwa unyofu wa moyo
Ndani ya nyumba yangu.
3 Yos 23:6; 1 Sam 12:20 Sitaweka mbele ya macho yangu
Neno la uovu.
Kazi yao waliopotoka naichukia,
Haitaambatana nami.
4 Mt 7:23; 1 Kor 5:11; 2 Tim 2:19 Moyo wa ukaidi utaondoka kwangu,
Lililo ovu sitalijua.
5 Mit 6:17; Lk 18:14 Amsingiziaye jirani yake kwa siri,
Huyo nitamwangamiza.
Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno,
Huyo sitamvumilia.
6 Rum 13:4 Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,
Hao wakae nami.
Yeye aendaye katika njia kamilifu,
Ndiye atakayenitumikia.
7Hatakaa ndani ya nyumba yangu
Mtu atendaye hila.
Asemaye uongo hatathibitika
Mbele ya macho yangu.
8 Yer 21:12; Hos 9:3 Kila asubuhi nitawaangamiza
Waovu wote nchini.
Nikiwatenga wote watendao uovu
Na mji wa BWANA.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.