Zaburi 14 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Kushutumiwa kwa wasiomwamini MunguKwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1 Rum 3:10-12; Zab 10:4; Mit 1:7,22; Mwa 6:12 Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu;

Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo,

Hakuna atendaye mema.

2Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu,

Aone kama yuko mtu mwenye hekima,

Amtafutaye Mungu.

3Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja,

Hakuna atendaye mema,

La! Hata mmoja.

4Je! Wote wafanyao maovu hawajui?

Walao watu wangu kama walavyo mkate,

Hawamwiti BWANA.

5Hapo ndipo waovu watakaposhikwa na hofu nyingi,

Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki.

6Mnaiharibu mipango ya mtu mnyonge,

Bali BWANA ndiye aliye kimbilio lake.

7Laiti wokovu wa Israeli ungetoka katika Sayuni!

BWANA awarudishapo wafungwa wa watu wake;

Yakobo atashangilia,

Israeli atafurahi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help