Isaya 36 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Senakeribu atishia Yerusalemu

1 toka Lakishi pamoja na jeshi kubwa kwenda hadi Yerusalemu kwa mfalme Hezekia. Naye akasimama karibu na mfereji wa bwawa la juu, lililo katika njia kuu ya kuuendea Uwanda wa Dobi.

3Wakamtokea Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu, mwenye kuandika kumbukumbu.

4Yule kamanda akawaambia, Haya, mwambieni Hezekia, kwamba mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru, asema hivi, Ni tumaini gani hili unalolitumainia?

5Nasema, mashauri yako, na nguvu zako kwa vita, ni maneno yasiyo na maana; basi, unamtumaini nani hata ukaniasi mimi?

6Eze 29:6-7 Tazama, unaitumainia fimbo ya mwanzi huu uliovunjika, yaani, Misri, ambayo, mtu akitegemea juu yake, humwingia mkononi na kumchoma; ndivyo alivyo Farao, mfalme wa Misri, kwa wote wamtumainio.

72 Fal 18:4 Lakini ukiniambia, Tunamtumaini BWANA, Mungu wetu, je! Si yeye ambaye Hezekia ameondoa mahali pake mlimoinuka, na madhabahu zake, akawaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, Sujuduni mbele ya madhabahu hii?

8Basi sasa, tafadhali mpe bwana wangu, mfalme wa Ashuru, dhamana, nami nitakupa farasi elfu mbili, ikiwa wewe kwa upande wako waweza kupandisha watu juu yao.

9Wawezaje, basi, kurudisha nyuma uso wa afisa mmoja wa watumishi walio wadogo wa bwana wangu, na kuitumainia Misri upewe magari na farasi?

10Je! Nimepanda mimi, ili kupigana na mahali hapa na kupaangamiza, bila shauri la BWANA? BWANA ndiye aliyeniambia, Panda upigane na nchi hii na kuiangamiza.

11Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, na Shebna, na Yoa, wakamwambia yule kamanda, Tafadhali, sema na watumishi wako kwa lugha ya Kiashuri; maana tunaifahamu; wala usiseme nasi kwa lugha ya Kiyahudi, masikioni mwa watu wote walio ukutani.

12Lakini yule kamanda akawaambia, Je! Bwana wangu amenituma niseme, maneno haya kwa bwana wako na kwako wewe? Hakunituma pia kwa watu hawa wanaokaa ukutani, wanaokabiliwa na tisho la kula mavi yao wenyewe na kunywa mkojo wao pamoja nanyi?

13Kisha yule kamanda akasimama akalia kwa sauti kuu kwa lugha ya Kiyahudi, akisema, Lisikieni neno la mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru.

14Mfalme asema hivi; Hezekia asiwadanganye, kwa maana hataweza kuwaokoa;

15wala msimwache Hezekia kuwatia moyo wa kumtumaini BWANA; akisema, BWANA bila shaka atatuokoa, mji huu hautatiwa katika mkono wa mfalme wa Ashuru.

16Mik 4:4; Zek 3:10 Msimsikilize Hezekia; maana mfalme wa Ashuru asema hivi, Fanyeni suluhu na mimi, mkatoke mnijie, mkale kila mtu matunda ya mzabibu wake na matunda ya mtini wake, mkanywe kila mmoja maji ya kisima chake mwenyewe;

17hata nije nikawachukue mpaka nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai, nchi ya mkate na mashamba ya mizabibu.

18Jihadharini, Hezekia asije akawadanganya, akisema, BWANA atatuokoa. Je! Kati ya miungu ya mataifa, kuna yeyote aliyewahi kuokoa nchi yake kutoka katika mkono wa mfalme wa Ashuru?

19Hes 34:8; Yos 13:5 Wako wapi miungu ya Hamathi na ya Arpadi? Wako wapi miungu ya Sefarvaimu? Je! Wameiokoa Samaria na mkono wangu?

202 Nya 32:15; Zab 50:21; Isa 37:23; Dan 3:15 Katika miungu yote ya nchi hizi ni nani waliookoa nchi yao kutoka katika mkono wangu, hata BWANA auokoe Yerusalemu kutoka katika mkono wangu?

21Zab 38:13; Mit 9:7; Amo 5:13; Mt 7:6 Lakini watu wakanyamaza kimya; wala hawakumjibu hata neno moja; maana ilikuwa amri ya mfalme, kwamba, Msimjibu neno.

22Mwa 37:34; 1 Sam 4:12; 2 Sam 1:11; 2 Fal 18:18,37; Ayu 1:20; Isa 33:7 Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu mwenye kuandika kumbukumbu, wakaenda kwa Hezekia, na nguo zao zikiwa zimeraruliwa, wakamwambia Hezekia maneno ya yule kamanda.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help