1 iliyo ya Wasidoni, mpaka Afeka, hata mpaka wa Waamori;
5 Wareubeni na Wagadi walipata urithi wao, waliopewa na Musa, huko ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki, vile vile kama huyo Musa mtumishi wa BWANA alivyowapa;
9Hes 21:30; Isa 15:2; Yer 48:18,22 kutoka huko Aroeri, iliyoko pale ukingoni mwa bonde la Amoni, na huo mji ulioko pale katikati ya bonde, na nchi tambarare yote ya Medeba mpaka Diboni;
10na miji yote ya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala katika Heshboni, hata mpaka wa wana wa Amoni;
11Yos 12:5 na Gileadi na mpaka wa Wageshuri, na Wamaaka, na mlima wa Hermoni wote, na Bashani yote mpaka Saleka;
12Kum 3:11; Hes 21:24 ufalme wote wa Ogu uliokuwa katika Bashani, huyo aliyekuwa akitawala katika Ashtarothi na katika Edrei (huyo alisalia katika mabaki ya wale Warefai); kwa kuwa Musa aliwapiga hao na kuwafukuza.
13Pamoja na hayo wana wa Israeli hawakuwafukuza Wageshuri, wala Wamaaka; lakini Wageshuri na Wamaaka wamekaa kati ya Israeli, hadi siku hii ya leo.
14Kum 18:1; 10:9; 12:12,19; Hes 18:20; Yos 14:3,4 Lakini hakuwapa watu wa kabila la Lawi urithi wowote ule; maana sadaka za BWANA, Mungu wa Israeli, zisongezwazo kwa njia ya moto ndizo urithi wake huyo, kama alivyomwambia.
Nchi ya Reubeni15Musa akawapa kabila la wana wa Reubeni kwa kadiri ya jamaa zao.
16Hes 21:28,30; Kum 3:12; Yos 12:2 Mpaka wao ulikuwa kutoka hapo Aroeri, iliyo pale ukingoni mwa bonde la Arnoni, na huo mji ulio katikati ya bonde, na nchi tambarare yote iliyo karibu na Medeba;
17na Heshboni na miji yake yote iliyoko katika bonde; na Diboni, na Bamoth-baali, na Beth-baal-meoni;
18Hes 21:23 na Yahasa, na Kedemothi, na Mefaathi;
19Hes 32:37 na Kiriathaimu, na Sibma, na Sereth-shahari katika kilima cha hilo bonde;
20na Beth-peori, na nchi za materemko ya Pisga, na Beth-yeshimothi;
21Kum 3:10; Hes 21:24; 31:8 na miji yote ya nchi tambarare, na ufalme wote wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akitawala katika Heshboni, aliyepigwa na Musa pamoja na hao wakubwa wa Midiani, nao ni Evi, na Rekemu, na Suri, na Huri, na Reba, hao watawala wa Sihoni, waliokuwa katika nchi hiyo.
22Hes 22:5; 24:1; 31:8; 2 Pet 2:15; Ufu 2:14 Balaamu naye, huyo mwana wa Beori, huyo mchawi, wana wa Israeli walimwua kwa upanga kati ya hao wengine waliowaua.
23Na mpaka wa wana wa Reubeni ulikuwa ni mto wa Yordani, na kingo zake. Huo ndio urithi wa wana wa Reubeni sawasawa na jamaa zao, miji yake na vijiji vyake.
Nchi ya Gadi24Musa akawapa kabila la Gadi, hao wana wa Gadi, kwa kadiri ya jamaa zao.
25Hes 32:35; 21:26-29; Kum 2:19; Amu 11:13; 2 Sam 11:1; 12:26 Mpaka wao ulikuwa ni Yazeri, na miji hiyo ya Gileadi, na nusu ya nchi ya wana wa Amoni, mpaka Aroeri uliokabili Raba;
26tena kutoka Heshboni mpaka Ramath-Mizpe, na Betonimu; tena kutoka Mahanaimu hadi mpaka wa Debiri;
27Mwa 33:17; 1 Fal 7:46; Hes 34:11; Kum 3:17; Yos 11:2; Mt 14:34; Lk 5:1 tena katika bonde, Beth-haramu, na Bethnimira, na Sukothi, na Safoni, hiyo iliyosalia ya ufalme wa Sihoni mfalme wa Heshboni, yaani mto wa Yordani na kingo zake, mpaka mwisho wa bahari ya Kinerethi ng'ambo ya pili ya Yordani upande wa mashariki.
28Huo ndio urithi wa wana wa Gadi sawasawa na jamaa zao, miji yake na vijiji vyake.
Nchi ya nusu kabila la Manase (mashariki)29Kisha Musa akawapa hao wa nusu ya kabila la Manase urithi wao; ulikuwa ni wa hiyo nusu ya kabila la wana wa Manase sawasawa na jamaa zao.
30Hes 32:41; 1 Nya 2:23 Na mpaka wao ulikuwa kutoka huko Mahanaimu, Bashani yote, na ufalme wote wa Ogu mfalme wa Bashani, na miji yote ya Yairi, iliyo katika Bashani, miji sitini;
31Yos 12:4 na nusu ya Gileadi, na Ashtarothi, na Edrei, hiyo miji ya ufalme wa Ogu katika Bashani, ilikuwa ni ya wana wa Makiri mwana wa Manase, kwa hiyo nusu ya wana wa Makiri sawasawa na jamaa zao.
32Hii ndiyo mirathi ambayo Musa aliigawanya katika nchi tambarare za Moabu, ng'ambo ya pili ya Yordani, kukabili Yeriko, upande wa mashariki.
33Hes 18:20; Yos 18:7; Kum 10:9; 12:12; 14:27,29; 18:1,2; Eze 44:28 Lakini Musa hakuwapa kabila la Lawi urithi uwao wote; yeye BWANA, Mungu wa Israeli, ndiye urithi wao, kama alivyowaambia.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.